loader
Picha

Rushwa ya Acacia yaburuza 7 kortini

WATU saba wakiwemo wathamini watatu wa serikali pamoja na mthamini Mkuu wa Serikali, Joseph Kleruu (59), wamefi kishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh bilioni 11.345 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

North Mara ni moja ya migodi inayomilikiwa na Kampuni ya Accacia. Watuhumiwa wengine ni pamoja na diwani wa Kemambo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rashid Bogomba (48), Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakunguru, Abel Nyakibari (68) na Mwenyekiti wa kijiji cha Kewanja Mtanzania Omotima (54). Wengine ni wathamini wa serikali Adam Yusuf (53) na Peter Mrema (37) na Mhasibu wa mgodi huo na raia wa Afrika Kusini, Matern Vande Walt (35).

Akisoma mashtaka hayo juzi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime Veronika Mgendi, Mwendesha Mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alidai kuwa washtakiwa hao walifunguliwa kesi za jinai namba 476/2018, 478/2018, 479/2018 na 474/2018.

Alidai kuwa Bogomba na Omotima wenye kesi namba 476/2018 wanadaiwa kuwa katika kipindi cha Januari, 2006 na Mei, mwaka huu walijipatia kiasi cha Sh bilioni 7.70 kwa njia ya rushwa ili kushawishi wananchi wa mgodi huo wa North Mara usihamishe Shule ya Nyabigena kwenda eneo lingine la Mrwambe.

Alisema katika kesi namba 478/2018 Maginga akiwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakunguru katika kipindi cha Januari, mwaka 2014 mpaka mwaka huu alishawishi na kupokea Sh milioni 966.68 kama fidia kutoka mgodi wa North Mara na kutowalipa wananchi wengine.

Alisema pia katika kesi namba 479/2018 watuhumiwa Thomas ambaye ni Mthamini Mkuu na Mshauri wa Serikali kutoka Makao Makuu katika kipindi cha Mei na Juni mwaka 2013 alipokea dola za Marekani 243,650.75 kutoka mgodi wa North Mara kama kishawishi cha kuwapa upendeleo katika uthamini wa mazao na mali za wananchi.

Kwa mujibu wa Swai hongo hiyo iiliwakandamiza wananchi wanaozunguka mgodi kupata haki zao. Lakini pia anadaiwa kupokea dola za Marekani 681.572 kama kishawishi kwa kutumia kampuni yake binafsi kwa kupewa kazi ya upimaji na uthamini mazao na mali za wananchi.

Alisema watuhumiwa wengine katika kesi ya jinai namba 475 /2018, Mhasibu wa mgodi huo Vuulen, akiwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha anadaiwa kushirikiana na Meneja wa Kitengo cha Ardhi cha mgodi huo Johanes jnnes Vn na kutoa Sh milioni 93.896 kwa Adam Yusuf.

Kwa mujibu wake Yusuf ndiye aliyekuwa Mthamini Mkuu katika kikosi cha kushawishi cha kutoa upendeleo kwa mgodi wa North Mara na anadaiwa kupokea fedha hizo kama rushwa ya kushawishi.

Aidha, alisema Mrema akiwa mthamini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anadaiwa kupokea Sh milioni 30 kama kishawishi kuwanyima wananchi haki zao na kutoa upendeleo kwa mgodi huo wa North Mara.

Watuhumiwa hao wote walikana mashitaka na kuomba dhamana ambapo wanasheria wa Takukuru, Swai na Yahaya Mwinyi walipinga dhamana na kusoma kifungu cha 148 (5) (e) na (d) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007.

Kwa mujibu wa Mwinyi dhamana ya watuhumiwa inapimwa na kiasi walichopokea na kuhujumu ambapo watuhumiwa wote hao wanatuhumiwa kupokea Sh bilioni 11 na dola za Marekani zaidi ya 800 hivyo hawastahili dhamana.

Hata hivyo, Hakimu Mgendi alitoa masharti ya dhamana kuwa wawe na wadhamini wawili wenye hati za mali zisizohamishika zikiwemo hati za nyumba zenye thamani ya Sh bilioni nne ambapo watuhumiwa hao walishindwa na kupelekwa mahabusu, hadi Oktoba 24, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Samson Chacha, Tarime

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi