loader
Picha

Walima chikichi kupata mbegu mpya

KATIKA kuhakikisha kiwango cha uzalishaji wa mafuta ya kula kinaongezeka nchini wataalamu wa utafi ti kupitia Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo (TARI) wameanza kuchukua hatua madhubuti ya kukabili suala hilo.

Kupitia mpango huo wataalamu hao wameweka mikakati ya kuhakikisha kilimo hicho kinaendelezwa kwa kutumia mbegu bora za chikichi aina ya tenela ambapo kwa mwaka wa kwanza wanategemea kuzalisha mbegu milioni 10 kati ya milioni 20 zinazotakiwa ndani ya miaka mitatu.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Geofrey Mkamilo kwenye kikao cha Manejimenti na wawakilishi wa wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Tari kilichofanyika jijini Dodoma.

Alisema uzalishaji wa chikichi unalenga kuzalisha mafuta ya kula ili kupunguza kiwango cha uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi. Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa taasisi hiyo pia imeweka mpango mkakati wa miaka mitano utakaowezesha kila kituo cha utafiti kuzalisha teknolojia bora za kilimo katika kila zao husika ili kuweza kumfikia mkulima na kuzalisha kwa tija.

Alisema alisema kuwa ndani ya miaka hiyo mitano TARI itaangalia kurugenzi mbili za kitaaluma zilizopo ikiwemo ile ya Kurugenzi ya Utafiti na Ubunifu na ile ya Usambazaji wa Teknolojia na Mawasiliano ili kuhakikisha zinafanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko katika Sekta ya Kilimo.

Alisema mkakati huo unalenga kila kituo cha utafiti kuwa na mazao yake ambayo kinayashughulikia, akitoa mfano wa Kituo cha Kibaha ambacho kinashughulikia utafiti wa zao la miwa.

Alivitaja vituo vingine kuwa ni pamoja na kituo cha Mikocheni ambacho kinashughulikia bioteknolojia na uendelezaji wa zao la minazi, Ilonga, Dakawa, Ifakara, Uyole, Naliendele Mtwara, Kihinga mkoani Kigoma, Ukiriguru Mwanza, Saliani Arusha na vinginevyo.

Akizungumzia suala la uzalishaji wa Michikichi kituoni kwake, Dk Kiddo Mtunda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI –Tumbi alisema kuwa wamejipanga kuzalisha miche bora ya chikichi itakayosambazwa katika mikoa yote inayolima zao hilo nchini.

Alisema hata hivyo kwa kuanzia miche hiyo itasambazwa katika mikoa ya Mbeya, Tanga, Pwani, Kigoma ambapo pia wamejipanga kuongeza uelewa kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu bora ili waweze kupata tija.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi