loader
Picha

Watu 5,000 wachunguzwa macho

KATIKA wiki ya maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho kwa mwaka 2018, watu 5,000 wamechunguzwa huku zaidi ya 200 wakifanyiwa upasuaji kutoka mikoa tisa.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk Bernadetha Shilio katka kuhitimisha kilele cha maadhmihso hayo.

Alisema kwa upande wa Mkoa wa Dodoma ambapo maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa, watu 368 wamefanyiwa uchunguzi na ushauri wa macho na magonjwa yasiyoambukiza kama sukari, shinikizo la damu na kiwango cha unene.

“Asilimia tatu wamekutwa na kiwango cha juu cha sukari, asilimia 47 wamekutwa na shinikizo la juu la damu, asilimia 50 wamekutwa na unene uliopitiliza kiwango na wote wamepewa ushauri na kuandikiwa dawa kwa waliostahili,”alisema.

Shilio alisema katika uchunguzi huo wamebaini kuwa bado jamii ya kitanzania haizingatii utunzaji wa afya ya macho na kuwataka kujenga na kuiga tabia chanya zilizo na tija kwa afya. “Watu wanaopaka rangi, wanja au kubandika kope kwenye kingo cha jicho wanahatarasha macho yao.

Utafiti wa mwaka jana kwa wagonjwa wa macho waliofika hospitalini asilimia kubwa ya wanawake walikuwa na matatizo ya kuvimba macho,”alisema. Naye, Mkuu wa Idara ya Macho katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Rajab Kisonga alisema tangu kuanza maadhimisho hayo, wamewafanyia upasuaji wa macho wagonjwa 28 huku wagonjwa 38 wakiwa kwenye foleni.

“Mpaka sasa wagonjwa 66 wako kwenye utaratibu wa kupewa tiba ya upasuaji wa macho, lakini idadi hii inaweza kuongezeka kwa sababu uchunguzi wa watu wengine bado unaendelea pale Viwanja vya Nyerere,”alisema.

Veronica Maganza alisema baada ya kuona umati wa watu kwenye viwanja vya Nyerere aliaamua kwenda kupima afya yake na ndipo walipobaini kuwa jicho lake la kulia ambalo lilikuwa zima nalo lina shida.

“Mwaka jana nilifanyiwa upasuaji kwenye jicho la kushoto, ila leo wamebaini hata la kulia lina shida hivyo niko kwenye foleni ya kufanyiwa upasuaji,” alisema. Kwa Mkoa wa Dodoma, upimaji wa macho umefanyika kwa siku tano ambapo mamia ya wakazi wa jiji hilo walijitokeza katika viwanja vya Nyerere kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi