loader
Picha

Cape Verde hawachomoki

LEO timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars itakuwa ugenini mjini Praia, Cape Verde kuvaana na wenyeji wao kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

Tayari kikosi cha Stars kimeshawasili visiwani humo tangu juzi kikiwa na ari kubwa ya kupambana na kupata ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu ili kuweka matumaini ya kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ilipofanyika Lagos, Nigeria.

Msimamo wa kundi lao unaonesha Uganda ndio vinara wakiwa na pointi nne, Lesotho ya pili wakiwa na pointi mbili sawa na Stars, lakini wanatofautiana kwa uwiano wa mabao na Verde wanaburuza mkia wakiwa na pointi moja.

Stars itaingia kwenye mchezo huo huku ikijua fika ina deni kubwa kwa Watanzania kutokana na maandalizi iliyofanywa. Rekodi zinaonesha kuwa timu hizi zimekutana mara mbili mwaka 2008 katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia ambapo Oktoba 11 Stars wakiwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 yaliyofungwa na Athuman Iddi ‘Chuji’, Jerson Tegete na Mrisho Ngassa, waliporudiana Cape Verde walishinda bao 1-0.

Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike alisema kuwa kikosi chake kipo kwenye hali nzuri na anafurahi zaidi kuona wachezaji wake ni wepesi katika kufuata maelekezo yake. Kikubwa kinachomuaminisha kocha huyo kufanya vizuri katika mchezo ulio mbele yake, wachezaji wake kufanya anachowafundisha.

“Timu ya taifa ni jambo la kujivunia kwa taifa zima, huwa unaacha klabu yako na kufanya uzalendo, nafurahi kuona wachezaji kila siku wananielewa na kufuata kile ninachowaagiza, tuzidi kumuomba Mungu aisaidie timu kupata ushindi katika mchezo wetu na Cape Verde,” alisema Amunike.

Baada ya mchezo huo, Stars italazimika kurudi nchini haraka kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Cape Verde ambao utapigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi