loader
Picha

MATOKEO DARASA LA 7: Mikoa 10 bora, shule zilizoongoza na kushika mkia hizi hapa

Baraza la Mitihani NECTA limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu huku matokeo yakionesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.96 ikilinganishwa na asilimia 72.76 mwaka 2017.

Akitangaza matokeo hayo Jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani, Dkt Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 walitunukiwa matokeo na wamefaulu huku watahiniwa 13, 686 sawa na asilimia 1.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo utoro na ugonjwa.

Baada ya taarifa hiyo ya utangulizi, sasa tuangalie Mikoa, Halmashauri, Manispaa na Majiji 10 yaliyofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo

1. Dar es Salaam  2. Geita 3. Arusha, 4. Kilimanjaro 5.  Kagera 6. Mwanza 7. Iringa 8. Mtwara, 9. Katavi 10. Njombe.

Kwa upande mwingine, shule 10 zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo ni pamoja na  Raskazone (Tanga), Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga), St Anne Marie (Dar es Salaam), Jkibira, St Akleus Kiwa nuka, St Severine, Rweikiza zote za mkoani (Kagera).

Hakuishia hapo, Katibu wa Baraza la Mitihani amezitaja pia shule 10 zilizofanya vibaya zaidi katika matokeo hayo. Shule hizi na mahali zilipo ni Mangika (Tanga), Mwazizi (Tabora), Isebanda (Simiyu), Malagano (Tabora), Magana (Mara), Kododo (Morogoro), Mtindili (Tanga), Lumalu (Ruvuma), Chidete (Dodoma), Mavului (Tanga).

Hata hivyo, Baraza pia limefuta matokeo yote ya watahiniwa 357 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao ya kumaliza shule ya msingi.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi