loader
Picha

Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

VIONGOZI 15 kutoka upinzani wilayani Temeke, wamekabidhi kadi zao kwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, baada ya kuvihama vyama vyao na kuhamia chama hicho tawala.

Hafla hiyo ya kupokea viongozi hao wa upinzani ilifanyika juzi na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM. Diwani wa Mtoni kwa Azizi Ally, Benard Mwakyembe aliyekuwa Chadema na kuingia CCM, ameahidi kurudisha CCM viti vyote vilivyokua upinzani.

"Nilikua napambana sana na Meya Abdallah Chaurembo, zaidi ya mara 10 tumekosakosa kutwangana makonde kwenye vikao vya madiwani, nimepambana sana na DC sasa nitapambania maendeleo ya wana Temeke, uchaguzi ujao nitagombea naomba wana Temeke msiniangushe," alisema.

Mbali na diwani huyo, Katibu Mwenezi wa ACT- Wazalendo ambaye amewahi kuwa Ofisa Uchaguzi Chadema kabla ya kutimkia ACT-Wazalendo, Steven Shekumkae akinukuu vifungu vya biblia, alidai ameoteshwa na Mungu arejee CCM.

"Mungu aliniotesha ule mstari wa enendeni mkaihubiri injili anayeamini ataokoka, mimi nimeokoka, nimezaliwa upya na wenzangu hali kadhalika sasa tukaitangaze CCM kwa mataifa yote," alisema.

Wengine waliorudisha kadi zao na nafasi zao kwenye mabano ni Amina Batash (Katibu ACT –Wazalendo Pwani, mjumbe Halmashauri Kuu), Abdul Kheri (Katibu Chadema kata ya Chang'ombe), John Matugura (Mwenyekiti Chadema Tuangoma), Charles Gahu ( Katibu kata na Mwenyekitu Bavicha Wilaya ya Temeke).

Said Mohamed (Chadema), James Nyaki ( Mwenyekiti Chadema Kata ya Kurasini), Mohammed Saidani (Chadema), Thomas Elius (Katibu Mwenezi kata ya Mtoni), Juma Said (Chadema) na Kelvin Abiud ( Mwenyekiti vijana ACT Wilaya ya Temeke).

Aidha, Edith Sebastian ( ACT baraza la wadhamini taifa), Ally Mbonde( Katibu wa Cuf, kata ya Tuangoma) na Renatus Lipambile (Mwenyekiti Chadema kata ya Kijichi) nao pia walihama vyama vyao na kutimkia CCM.

Akipokea kadi za wanachama hao wapya, Polepole aliwataka wana CCM kuwapa ushirikiano wanachama hao wapya na kuongeza kuwa bado nafasi zipo kwa watakaotaka kurejea wafanye hivyo kabla ya kufunga dirisha la usajili Desemba 31 mwaka huu.

"Kadi milioni mbili mpya zimeshawasili na Dar es Salaam peke yake kadi 13,000 zimeshatolewa,” alisema.

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo kwa tiketi ya CCM alisema kuwa Temeke ina majimbo mawili Mbagala na Temeke, na katika hayo Temeke ina kata 13 , CCM kata saba na upinzani kata sita.

Wakati Mbagala kuna kata 10 CCM kata saba na upinzani kata tatu zote zikiwa za CUF, serikali za mitaa jumla ni 142, CCM mitaa 102, upinzani 40 kwa Wilaya yote ya Temeke. Kampeni za madiwani na ubunge zinatarajiwa kuanza Novemba 4, kata 26 zitagombewa, wakati ubunge majimbo yatakayowaniwa ni Simanjiro, Serengeti na Babati.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi