loader
Picha

Amber Rutty ashtakiwa kwa mapenzi kinyume cha maumbile

VIDEO Queen, Rutyfi ya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake, Said Mtopali, wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.

Mbali ya hao, mshitakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama James Delicious, aliyesomewa mashitaka ya kuchapisha video au picha za ngono na kuzisambaza katika makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwezire. Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga alidai kuwa mashitaka ya kwanza yanamkabili Amber Rutty ambaye anadaiwa kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.

Pia alidai kuwa kati ya Oktoba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa Amber Rutty alimruhusu Said Mtopali kumuingilia kinyume cha maumbile, jambo ambalo ni kinyume na sheria. Katuga alidai kati ya Oktoba 25, mwaka huu, maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, alifanya mapenzi kinyume cha maumbile na mshitakiwa Amber Rutty.

Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Oktoba 25, mwaka huu, James Delicious alisambaza video za ngono kupitia makundi ya WhatsApp. Pia inadaiwa katika mashitaka ya nne kuwa Oktoba 25, mwaka huu Amber Rutty na Mtopali walisambaza picha za ngono kupitia makundi ya WhatsApp.

Washitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kwani wanasubiri taarifa za kitaalamu kuhusu picha za mnato za ngono. Hakimu Rwezile aliwataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Taifa, watakaosaini kulipa bondi ya Sh milioni 15.

Pia aliwataka washitakiwa hao kuwasilisha hati zao za kusafiria na kuwataka wasitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na ruksa. Hata hivyo, mshitakiwa James Delicious yeye peke yake ndiye aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Mtopali wakishindwa kutimiza masharti na kupelekwa gerezani. Hakimu Rwezile aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: ncisca Emmanuel

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi