loader
Picha

Shime alia na Kagere

KOCHA wa JKT Tanzania, Bakari Shime amesema mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amekuwa wa kwanza kuharibu rekodi yao kwa msimu huu baada ya kufunga mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga juzi.

Akizungumza jana, Shime alisema huu ni mchezo wa 11 wakicheza na walikuwa hawajafungwa ila Kagere ameharibu rekodi yao, kwani bao la kwanza kufunga liliwatoa mchezoni na kupoteza umakini.

“Kagere alifunga bao la kwanza dakika ya 13 ambalo lilikuwa jepesi na aliongeza la pili dakika ya 39 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Abdulrahman Mohamed na kufanikiwa kuharibu rekodi yetu kwani tangu ligi ianze hatujaruhusu bao kipindi cha kwanza,” alisema Shime.

Pia Shime amesema wanajiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Novemba 8 na kuhakikisha wanafanya vizuri baada ya makosa waliyofanya katika mechi dhidi ya Simba.

Simba kwa sasa imefikisha pointi 26 nyuma ya Azam FC wenye pointi 27 na JKT wamefikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 12 na kushika nafasi ya saba.

TIMU nne zinazopeperusha bendera ya nchi kimataifa kwenye Ligi ya ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi