loader
Picha

Kocha Alliance afurahia ushindi

KOCHA wa muda wa timu ya Alliance FC, Daddy Gilbert amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Martin Kigii katika dakika ya 90 baada ya kuunganisha vyema pasi ya Godlove Mdumule.

Ushindi huo umeipandisha Alliance FC mpaka nafasi ya 17 ikiwa na alama 10 baada ya michezo 13. Daddy Alisema timu yake ilicheza vyema na ilifanikiwa kutawala mchezo huo katika vipindi vyote.

Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanashinda michezo yote ya ligi iliyopo mbele yao.

Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza wajitokezee kwa wingi katika kusapoti timu hiyo, ambayo inashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliochezwa mkoani Mara juzi katika Uwanja wa CCM Karume, wenyeji Biashara United walilazimisha sare ya bila kufungana na Mbao FC.

Kocha wa msaidizi wa Biashara United, Omary Madenge alisema timu yake ilicheza vizuri lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizotengeneza.

Kocha Mkuu wa Mbao FC, Amri Saidi `Stam’ alisema atajipanga upya ili timu yake ipate ushindi dhidi ya timu ya Ndanda FC katika mchezo wao ujao.

TIMU nne zinazopeperusha bendera ya nchi kimataifa kwenye Ligi ya ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi