loader
Picha

Hakikisha ulinzi, usalama wa wateja

NI kweli tunafanya biashara ili tupate pesa, ni kweli pia kuwa wateja tunao wahudumia wana wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wao na mali zao wanazozinunua kutoka kwetu, lakini je, wanapoumizwa au bidhaa zao kuibwa ndani ya maduka yetu tunakosa kuhusika kuondoa ubaya wowote uliotokea?.

Swali hili lina maana pana na kwa namna moja au nyingine, linatukumbusha kuwa ulinzi na usalama wa mteja na bidhaa zake hasa awapo katika eneo letu la biashara ni jukumu linaloweza kutuhusu wafanyabiashara na wala si kuliacha kwa mteja pekee.

Suleiman Kashmir au Dulla G kutoka Geita ameniandikia ujumbe mrefu akiuliza iweje mteja alipie bidhaa, aipokee na kuipoteza baadaye ndani ya duka lake halafu ahusishwe kuhakikisha inapatikana? Kashmir anasema, anachofahamu ni kwamba kabla hajapokea fedha ya malipo ya bidhaa anayoiuza ambayo mteja ameipenda, anakuwa na wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wake, lakini si baada ya mteja kuilipia.

Anahoji: “Sasa nitaangalia usalama wa bidhaa zangu na za mteja kwa sababu zipi wakati mteja anajua kabisa kilicholipiwa si cha muuzaji tena?” Anamalizia kwa kusema kuwa anachokiona ni usumbufu na njia hasi ya wateja kutaka kulipwa pindi wapotezapo bidhaa zao kwa uzembe. “Mimi nawaambia kabisa wateja wangu wachunge bidhaa zao kwa sababu nanijua, kulipa madeni yatokanayo na uzembe wa mtu ni tatizo kubwa kwangu”.

Kwa ufupi, ulinzi na usalama wa mteja unazungumziwa na wataalamu mbalimbali wa masuala ya biashara katika mitandao miwili; wa maswali (www.ask.com na wa majibu www.answers.com) kwa maneno tofauti lakini yanayoleta maana moja ambayo ni suluhisho kwa tatizo tunalolizungumzia leo.

Naliita tatizo kwa sababu tayari limeleta maswali na mashaka endapo mfanyabiashara anawajibika kuhakikisha usalama wa mteja wake na bidhaa zake au la, huku wengine wakiamini kwamba ni wajibu na wala si ombi katika maeneo fulani mteja kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake na bidhaa zake.

www.ask.com, inahoji: “Je, suala la kuhakikisha mteja unayemuuzia sambusa hapati zenye sumu ni la Polisi? au nila mamlaka zinazohusika kusimamia afya mitaani? Je, mamlaka hizo zinakuwepo wakati wa maandalizi ya sambusa zinazotayarishwa iki kuuzwa dukani au mgahawani kwako?” www.answers.com nayo inahoji: “Anayepaswa kuulizwa kuhusu kupotea kwa bidhaa zangu ndani ya duka lako ni nani ikiwa hukujishughulisha kuhakikisha usalama wangu pamoja na mizigo yangu?

Utaniuziaje bidhaa. Kwa jumla, muuzaji au mmiliki wa duka, biashara ambako bidhaa ya mteja inaibwa, hata kama mteja amekwishailipia, hana namna ya kukwepa kuhusika kuulizwa kuhusu upotevu huo, kwa sababu unakuwa umetokea katika himaya yake. Kimsingi, mfanyabiashara anapaswa kuhakikisha mteja anaondoka salama kwenye eneo lake, bila kupata usumbufu wa aina yoyote ikiwemo huo wa bidhaa kuibwa.

Mtandao wa wwww.ask.com, unasema mfanyabiashara apatapo malalamiko ya upotevu wa bidhaa au kuibwa kwa bidhaa iliyonunuliwa dukani kwake, zipo namna mbalimbali ikiwemo kuanzisha msako wa haraka katika mazingira ya biashara husika kabla wateja wengine wote hawajatoka. Kadhalika, anaweza kuwa amechukua tahadhari kwa kufunga kamera katika eneo lake au kuweka walinzi watakaokuwa maalumu kuhakikisha mteja mmoja haondoki na bidhaa isiyo yake.

Maduka mengi katika miji iliyoendelea mfano Dar es Salaam yana utaratibu huu. Anayetoka na mzigo anaonesha risiti ya malipo kwa mlinzi aliyeko mlangoni. Vinginevyo, www.answers inasema, mfanyabiashara atalazimika kufanya ufuatiliaji au kuisaidia Polisi katika uchunguzi kuhakikisha wezi wanapatikana au bidhaa inapatikana.

Hakuna namna mfanyabiashara anayeweza kukwepa kuhusika kuhakikisha usalama wa bidhaa ya mteja iliyonunuliwa dukani kwake na kuibwa ndani ya maeneo ya duka lake. “Zaidi ya hapo, kuleta ubishi mwingi kutadhihirisha kuwa mfanyabiashara au mfanyakazi katika biashara hiyo anahusika kusababisha wizi wa bidhaa ya mteja,” www. answers.com inasema.

Wanaofanya biashara ya vyakula wanapaswa pia kuhakikisha mazingira ya biashara nayo ni safi wakati wote. Www.ask.com inasema, katika kila nchi kuna viwango vya ubora vya ubora bidhaa zikiwemo za vyakula na zile zenye uwezo wa kuathiri maisha ya mteja moja kwa moja kama vile vipodozi na nyinginezo. Katika hilo, mtandao huo unashauri ulinzi na usalama wa mteja uhakikishwe na mfanyabiashara kwa kuzingatia viwango vya ubora.

KATI ya nchi zinazokuja kwa kasi katika kuboresha sekta ya ...

foto
Mwandishi: Namsembaeli Mduma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi