loader
Ajali yaua wanandoa saa mbili baada ya harusi

Ajali yaua wanandoa saa mbili baada ya harusi

MAHARUSI wawili wameibua hisia za watu mbalimbali nchini Marekani hivi karibuni baada ya kupata ajali ya helikopta na kufariki takribani saa mbili tu baada ya kufunga ndoa.

Inaelezwa kuwa wawili hao, Will na Bailee Byler walifunga ndoa yao jioni ya Jumamosi, wiki iliyopita, nyumbani kwa familia ya bwana harusi katika eneo la Texas Kaskazini.

Mara baada ya harusi wanaelezwa kuwa walipanda na kuondoka na helikopta hiyo iliyokuwa ikiongozwa na rubani, Gerald Lawrence, ambaye pia ametajwa kufariki dunia baada ya ajali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, helikopta hiyo ilipata ajali katika eneo la lakini hata hivyo walifanikiwa kuipata siku ya Jumapili asubuhi.

Watu mbalimbali wametumia mitandao yao ya kijamii kutoa pole kwa familia za wafiwa, huku wakiandika jinsi gani wameguswa na kifo cha wanandoa hao wachanga.

Wawili hawa walikuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sam Houston State.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8f93abf99e227848861f7143794ca61a.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Post your comments