loader
Picha

Uyui yazikaribisha benki, hoteli, sheli

Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gift Msuya amesema, kwenye wilaya hiyo kuna maeneo makubwa ya uwekezaji hivyo wananchi waende kuitumia fursa hiyo.

Amesema ofisini kwake kuwa wanahitaji wawekezaji kwenye maeneo ya utoaji huduma vikiwemo vituo vya mafuta, benki, hoteli, masoko, vituo vya mabasi, sehemu za watu kupumzika.

“Tunahamasisha watu wetu waje kuwekeza kwenye maeneo hayo kwa sababu huduma nyingi za msingi tunazipata Tabora manispaa kwa sasa” amesema Msuya wakati anazungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo mkoani Tabora kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo.

Amesema, baadhi ya kata zimeshatenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji zikiwemo za Goweko, Sikizya, Ilolangulu, Kigwa, Miyenze, Loya na Bukumbi.

“Mpaka sasa Halmashauri yetu haina hata kituo kimoja cha mafuta, haina maduka, haina hoteli kwa hiyo ni hitaji kubwa ambalo tunafikiri ni muhimu sana kwa ajli ya huduma kwa wananchi wetu” amesema Msuya.

Amesema, wilaya hiyo pia ina maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa ranchi za mifugo.

“Wilaya mpaka sasa ina ng’ombe wapatao 441,090 lakini hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuanzisha ranchi. Maeneo makubwa yametengwa kama hifadhi kwa hiyo tunafikiria tukiazisha ranchi inaweza kuwa ni msaada kwa wakulima kwa ajili ya kuongeza lakini pia kwa Halmashauri kama chanzo kimojwapi cha mapato ya Halmashauri” amesema.

Amesema, Wilaya hiyo inahitaji uwekezaji kwenye machinjio ya kisasa.

“Lakini pia tunahitaji uwekezaji kwenye kiwanda cha kusindika ngozi, tuna wafugaji wengi na ngozi nyingi huwa wafugaji wakishapeleka pale ng’ombe zikichinjwa na kuuzwa ngozi huwa zitupwa au zinazikwa kwa sababu hatuna utaalamu wa kuzichakata na kuzitengeneza ili ziweze kutengeneza bidhaa nyingine. Kwa hiyo tunahitaji kiwanda cha kuiongezea thamani ngozi na bidhaa za ngozi” amesema.

Amesema, kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, na kwamba, hamashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) ipo kwenye mchakati wa kuyapima na kuyapatia hati.

UBANDIKAJI wa majina ya wakulima wote wa korosho kwenye mbao ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Uyui

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi