loader
Picha

Simba kujenga sekondari

KLABU ya Simba baada ya kupata uongozi mpya inatarajia kuboresha miundombinu mbalimbali, ikiwemo kujenga shule ya msingi na sekondari kwa ajili ya kukuza vipaji vya soka.

Akizungumza Dar es Salaam mmoja wa wajumbe wapya wa Bodi ya Ukurugenzi wa klabu hiyo Mwina Kaduguda alisema wanataka kufuata nyayo za Ulaya, kwa kutengeneza vituo na shule za soka ili kutafuta vipaji.

Alisema wanataka baada ya miaka kadhaa kuwe na wachezaji waliowaivisha wenyewe watakaosaidia timu hiyo baadaye. “Tunataka Simba itoke kwenye ukongwe na iwe klabu kubwa, ni lazima tujenge miundombinu ya kisasa kama viwanja, gym, hosteli na tuwe na shule kutengeneza vikosi kwa umri tofauti ili mwisho wa siku tuwe na akina Lionel Messi (mchezaji wa Barcelona) na Sergio Ramos (Mchezaji wa Real Madrid) waliotengenezwa kwetu,” alisema.

Kaduguda alisema ujenzi wa shule hizo utaenda sambamba na viwanja kwa kila rika kutoa nafasi kwa vijana wengi wenye vipaji kupata fursa ya kukuzwa kisoka na kuendelezwa kielimu.

Hata hivyo, suala hilo ni mikakati ya baadaye kwani bajeti ya klabu hiyo ya mwaka 2018/2019 haijalitaja. Kwa sasa wekundu hao chini ya mwekezaji wao Mohamed Dewji wameshaanza ujenzi wa uwanja wa mazoezi Bunju ambao kwa mujibu wa bajeti ya msimu huu, inaonyesha utatokana na ufadhili wa Kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited (METL) utakaogharimu Sh milioni 200.

Baadhi ya wanachama waliohudhuria mkutano mkuu wao uliofanyika hivi karibuni, walipendekeza uwanja huo wa Bunju usiwe tu sehemu ya mazoezi bali itapendeza kama utaboreshwa na kuwa uwanja wao wa michezo.

Kaduguda ataungana na viongozi wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo mwishoni mwa wiki iliyopita kuisimamia Simba iliyobadilishwa kuwa Kampuni. Waliochaguliwa ni Mwenyekiti Sued Mkwabi na wajumbe ni Asha Baraka, Hussein Kitta, Dk Zawadi Kadunda na Selemani Haroub.

Mbali na hao, Simba pia ilimwajiri Mtendaji Mkuu Crescentius Magori aliyeahidi kuifanya Simba izungumzike Afrika. Jukumu alilopewa Magori ni kuhakikisha Simba inakuwa klabu ya mfano kwa kufanya vizuri ndani na nje, kutetea taji la ligi na kuchukua ubingwa wa Afrika.

TIMU nne zinazopeperusha bendera ya nchi kimataifa kwenye Ligi ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi