loader
Picha

‘Huwezi kujuta kuwekeza Kaliua’

Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imesema, yeyote anayekwenda kuwekeza huko hawezi kujuta.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dk. John Pima amesema ofisini kwake kuwa, wilaya hiyo yenye eneo la kilomita za mraba 14, 050 ni moja ya Halmashauri nane za Mkoa wa Tabora na ni miongoni mwa maeneo bora zaidi kuwekeza nchini Tanzania.

“Tuna malighafi za aina mbalimbali, mtu anaweza aje kukusanya tu malighafi, anaweza kuwa agent (wakala) tu wa malighafi, malighafi zipo za kutosha, ziko nyingi, lakini tuna asali kwanza. Kulingana na jiografia niliyoisema, asali yetu ya Wilaya ya Kaliua na Mkoa wa Tabora ni nzuri sana, ni one of the best honey” amesema Dk. Pima.

Kwa mujibu wa Dk. Pima, wanunuzi wakubwa wa asali ya Kalia ni Wabelgiji, na kwamba wanunuzi hao walifanya utafiti na wakajiridhisha kuwa, asali ya hapo ni bora zaidi kuliko nyingine wanayokusanya.

Amesema, kuna vyama vya ushirika vya ufugaji wa nyuki hivyo wanunuzi hao wanakwenda kuinunua kwa wakulima.

“Kwa hiyo mtu anayetaka kuinvest (kuwekeza) kwenye mazao ya asali na asali yenyewe ni eneo zuri sana, mapori yapo na ni rahisi tu kuweza kuinvest”amesema Dk. Pima.

Kwa mujibu wa Dk. Pima, kiwango cha asali inayosalishwa Kaliua ni kidogo kuliko mahitaji ya soko hivyo watu waende kuwekeza kwa kuwa kunaa soko la uhakika. Amesema, hivi sasa ni vigumu kupata asali katika eneo hilo kwa kuwa mahitaji ni makubwa kuliko iliyopo.

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa kujengwa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kaliua

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi