loader
Picha

Mkurugenzi- Kilimo Kaliua kinalipa sana

Sekta ya kilimo inalipa sana wilayani Kaliua, imefahamika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Dk. John Pima amesema, zao kubwa la Kaliua ni tumbaku na kwamba, wilaya hiyo ni Mkoa wa Tumbaku nchini Tanzania.

“Tumbaku kwa Tanzania, yaani mtoaji mkubwa wa tumbaku kwa Tanzania ni Kaliua. Yaani Wilaya ya kwanza kwa tumbaku Tanzania ni wilaya yetu na ndiyo maana tuna hadhi, tuna status ya Mkoa wa Tumbaku, kama Wilaya tunaitwa Mkoa wa Tumbaku”amesema.

Ametoa mwito watu wakawekeze kwenye kilimo ha tumbaku na kwamba, zao hilo halimtupi mkulima.

“Yaani hata hali iweje watapata vizuri sana kuliko mazao mengine” amesema Dk. Pima na kwamba, maeneo yapo ya kutosha na tayari mandalizi yamefanywa kufanikisha uwekezaji huo kwa wawekezaji wa ndani na wa kutoka nje.

Amekaribisha pi watu wakawekeze kwenye kilimo cha mpunga na kwamba Kaliua inazalisha kwa wingi zao hilo.

“Ni mwingi, maeneo mabonde ni mengi sana, kwa hiyo waje wainvest (wawekeze) pia kwa upande wa mpunga. Lakini tuna mazao mengine kama mazao ya mahindi na mazao mengine yanayochanganywa kama maharage, karanga, na yenyewe yanapatikana kwa wingi Kaliua” amesema.

Kwa mujibu wa Dk. Pima Halmashauri hiyo imeandaa utaratibu ili mwekezaji akisema anahitaji kiasia fulani cha ardhi kuwekeza kwenye kilimo anatimiziwa haja yake na kuna timu ipo kwa ajili hiyo.

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa kujengwa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kaliua

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi