loader
Picha

Kasi hii SGR inatia moyo

HABARI kwamba mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umefi kia asilimia 34 inaleta matumaini makubwa kwa watanzania walio wengi ambao wanaisubiri kwa hamu.

Kumekuwepo na umakini mkubwa katika kazi hii kutoka kwa wakandarasi ambao kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa aliyezungumza na gazeti hili juzi, wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanafikia lengo la muda wa kumaliza mradi huo mapema iwezekanavyo.

Mbali na mradi huo wa Dar hadi Morogoro kufikia hatua hiyo, pia Awamu ya Pili ya kutoka Morogoro hadi Makutupora imefikia asilimia nne. Tunaamini, kasi hiyo ambayo wakandarasi wameionesha katika kipindi hiki tangu kuwanza kwa mradi huu, haitakuwa nguvu ya soda, bali ni dhamira sahihi ya kwenda na kasi ya serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ambayo ina dhamira dhati ya kuwaletea watanzania maendeleo na kuwaondoa katika umasikini.

Kadogosa anasema mpaka sasa hali ya mradi ni shwari na wakandarasi wanajitahidi kwa uwezo wao wote kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kulingana na mkataba unavyosema.

Nia ya serikali ni kuona mradi huu wa Dar es Salaam hadi Morogoro wa kilometa 300 unatakiwa kukamilika mwaka 2019 na huu wa Morogoro hadi Makutupora unatarajiwa kukamilika Februari 2021 unakamilika kwa wakati.

Waswahili wanasema penye nia pana njia, kwa kuwa wakandarasi wanafanya kazi kwa bidii huku vifaa vinavyohitajika kuufanya mradi huo ukamilike kwa wakati, tuna kila sababu ya kuwapongeza kwanza kwa umakini wao, lakini pia kwa nia njema ya kuiaminisha jamii ya watanzania wenye shauku ya kuona mabadiliko ya kweli. Tunaposema uchumi wa viwanda Tanzania mpya unawezekana unadhihirishwa na kasi katika kuwezesha usafiri katika maeneo yote iwe ni kwa kutumia reli, barabara, anga na majini miundombinu yake inakuwa rahisi kwa watumiaji.

Tumeona jitihada za serikali katika ununuzi wa ndege mpya, vivuko katika maziwa mbalimbali nchini, matengenezo ya barabara hasa zinazounganisha nchi yetu na nchi za jirani, mikoa na wilaya. Itoshe kusema, wananchi ambao miradi hii inapitia wawe na mashikamano na wasiibe vifaa vya ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutakuwa kunarudisha nyuma ari na moyo kwa watendaji wa miradi hii muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi wote kwa ujumla.

IDADI ya majeruhi wa ajali ya lori la mafuta lililopinduka ...

foto
Mwandishi: HabariLeo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi