loader
Picha

Wasanii wakaribishwa kuiga 'ujanja' wa Wachina

WASANII nchini Tanzania wamekaribishwa kwenye maonyesho ya sanaa ya watu wa China ili waweze kupata ujuzi zaidi wa kazi wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuongeza maarifa.

Ofisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Habibu Msami amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo yatakayofanyika siku mbili katika Kituo cha Utamaduni wa Kichina jijini Dar es Salaam.

Msami alisema kwenye maonyesho hayo ya wasanii kutoka nchini China kuna kazi nzuri ambazo wasanii wa Tanzania wanaweza kujifunza ambazo zipo katika viwango vya hali ya juu.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza alisema hayo ni matunda ya uhusiano mrefu uliopo baina ya Tanzania na nchi ya China.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi