loader
Picha

Viongozi wakwepa kujaza wenza wao tamko la mali

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema sio viongozi wote nchini ni waaminifu, kwani hata katika jedwali la wenza katika fomu ya matamko ya mali zao, hawalijazi.

Aidha, imesema viongozi wengine hawataki taarifa zao za mali kupelekwa kwa wenza wao, jambo linaloonesha kuwa kuna tatizo kutoka ndani kwa viongozi hao. Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Jaji mstaafu Harold Nsekela alisema hayo jijini Dar es Salaam jana na kuwahimiza viongozi hao, kupeleka haraka taarifa zao kwa kuwa Desemba 31 ndio mwisho.

Kuhusu kama taarifa za matamko zinazopelekwa na viongozi hao ni za kweli, Jaji Nsekela alisema kuna tatizo katika eneo hilo, na viongozi sio wote waaminifu. “Kwa mfano lile tamko kuna sehemu ya wenza wengine hawajazi, kuna wengine na hili tumelikuta tulipoenda kuhakiki, mtu na mwenza wake lakini wanaelekeza kuwa tarifa hizi usimwambie mwenzangu,” alisema Jaji Nsekela na kufafanua kuwa maana yake toka ndani kuna tatizo.

Alisema maeneo mengine hawezi kusema kwa kuwa mengine ni ya siri. Kuhusu muda wa kurejesha taarifa zao, alisema inatakiwa hadi kufikia Desemba 31 kuwa tayari wamewasilisha matamko yao kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Aliwahimiza viongozi hao kurejesha matamko yao kwa sasa kwa kuwa ni tamko la mwaka, na viongozi wengi wana tabia ya kungojea tarehe za 25 ama 26 ndio hurejesha. Jaji Nsekela alisema matamko ya viongozi hao huainisha katika fomu hiyo na baadae ukaguzi wa mali hizo, uliofanywa na sekretarieti hiyo kwa lengo la kuhakiki kilichojazwa katika fomu hizo. Alisema baada ya kurejesha matamko hayo, huwatembelea viongozi mbalimbali kwa lengo la kujiridhisha na kile walichokijaza katika fomu zao.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi