loader
Picha

Magereza mapya 52 kujengwa

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti nchini.

Masauni aliyesema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rorya, Lameck Airo (CCM). Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga gereza la Wilaya ya Rorya hasa baada ya kuwa kanda maalumu ya kipolisi.

Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti likiwemo eneo la Rorya lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha. Alisema Wilaya ya Rorya ni miongoni mwa wilaya 52 nchini zisizo na magereza.

Aidha kutokana na ufinyu wa bajeti, serikali itaendelea na ukamilishaji wa magereza ambayo ujenzi wake umekwishaanza ambapo kipaumbele ni kuhakikisha inakamilisha miradi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi