loader
Picha

Ndugai ataka majibu ya kina upandishaji madaraja watumishi

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameagiza swali la upandishaji madaraja watumishi wa umma lirudiwe kuulizwa tena Alhamisi ijayo kutokana na kutoridhishwa na majibu yaliyotolewa na serikali.

Ndugai alitoa agizo hilo jana baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Josephat Kandege kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lupembe, Joram Hongoli (CCM) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora.

Katika swali lake la nyongeza, Hongoli alitaka kujua sababu za kutopandishwa madaraja watumishi walioajiriwa mwaka 2012. Naibu Waziri Kandege alikiri kuwa kuna wakati imetokea wale walioajiriwa pamoja ambao walistahili kupanda kwa pamoja wamekuwa hawapandi kwa pamoja.

Alisema hali hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo masuala ya kiutumishi ambayo yanapaswa kutimizwa. Aidha, Kandege alisema kumekuwa na malalamiko kuchelewa kupanda vyeo ambayo yanachangiwa na maofisa utumishi kwenye halmashauri hawatimizi wajibu kwa wakati. Alisema kuwa kwa mwaka 2012/13 jumla ya watumishi wa umma 37,388 waliajiriwa na kwa mujibu wa miundo ya utumishi, watumishi hao walitakiwa kuwa kwenye kipindi cha majaribio kwa muda wa mwaka mmoja. “Hadi kufikia mwaka 2013/14 walitakiwa kutumikia cheo kimoja kwa kipindi angalau miaka mitatu baada ya kuthibitishwa kazini, Watumishi hao walistahili kupandishwa madaraja kuanzia mwaka 2016/17 iwapo wangekidhi sifa muhimu za kimuundo kama utendaji mzuri wa kazi, kukidhi matakwa ya miundo husika ya mendeleo ya utumishi, kuwepo kwa nafasi wazi pamoja na uwepo wa bajeti iliyoidhinishwa,” alisema. Aidha, Kandege alisema watumishi hao pamoja na watumishi wengine hawakuweza kupandishwa kutokana na serikali kutekeleza uhakiki wa watumishi hewa na vyeti vya elimu ya sekondari na ualimu. Alisema baada ya kukamilika kwa uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti, serikali imewapandisha madaraja watumishi ikiwemo walioajiriwa mwaka 2012/13 kwa awamu. Kandege alisema awamu ya kwanza ilihusisha upandishaji vyeo watumishi 28,049 waliokuwa wameidhinishiwa vyeo vyao kabla ya kutekeleza uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti kuanzia juni, 2016. “Awamu ya pili ilianza Novemba 2017 na ilihusisha watumishi 59,967 ambao taarifa zao zilikuwa kwenye mfumo shirikishi wa Taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS)kabla ya zuio,” alisema. Alisema pia awamu ya tatu ilianza Aprili 2018 na ilihusishwa watumihsi 25,504 ambao barua zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye mfumo tajwa.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi