loader
Picha

Mbunge ataka watoto waliotelekezwa waasiliwe

MBUNGE wa Viti Maalum, Fatma Toufi q (CCM) amehoji kama serikali haioni umuhimu kuwaasili watoto waliotelekezwa. Akiuliza swali jana bungeni, Toufiq alidai kwamba watoto wengi wametelekezwa na wazazi wao na kuachwa wakizagaa mitaani.

“Je, serikali haioni kuwa sasa umefika wakati kuhamasisha jamii kuwaasili watoto hao ili nao wafaidike na malezi ya jamii,” aliuliza. Akijibu kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Utalii na Maliasili, Dk.Hamisi Kigwangala alisema matunzo na ulinzi wa mtoto ni haki ya mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.

Dk Kigwangala alisema kifungu cha 8 na 9 kinatoa majukumu kwa mzazi ama mlezi na mtu yeyote mwenye jukumu la kumlea mtoto kuhakikisha anawatunza ipasavyo watoto wake ikiwemo kuwapatia huduma za msingi kama chakula, malazi, mavazi na elimu.

“ Kifungu cha 14 cha sheria ya mtoto kinatoa adhabu kwa mlezi ama mzazi yeyote atakayekiuka kifungo hicho kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.”

Alisema kwa mujibu wa taarifa ya utafiti ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ya mwaka 2018, kuna jumla ya watoto 6,393 ikiwa ni wanawake 1,528 na wanaume 4,865 walitambuliwa katika mikoa sita.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi