loader
Picha

Apigia debe bajeti zaidi magazeti TSN

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) mkoani Tabora, Said Ntahondi ameiomba serikali kuu kuangalia uwezekano wa kuziwezesha wizara zote nchini kutenga bajeti kidogo kwa ajili ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ili itekeleze kwa weledi zaidi majukwaa ya biashara katika mikoa mbalimbali.

Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa Tanzania inazo fursa lukuki za kibiashara na uwekezaji ambazo hazijaibuliwa na kutangazwa, lakini kupitia ubunifu wa TSN, sasa fursa nyingi zinanadiwa na hivyo kuvutia uwekezaji nchini.

Alisema hayo jana mjini Tabora alipozungumza na timu ya waandishi wa habari kutoka TSN inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo kuhusu maandalizi ya Jukwaa la Biashara Tabora linalotarajiwa kufanyika Novemba 21 hadi 24, mwaka huu.

Alisema kupitia jukwaa hilo tayari fursa za Halmashauri ya Uyui ikiwemo uzalishaji wa mpunga bora, asali yenye ubora wa kipekee, kilimo cha mazao mengine ya biashara ikiwemo tumbaku, pamba, korosho na mifugo zimeanza kubainishwa kwa ajili ya uwekezaji mkubwa.

Alitaja fursa nyingine za Uyui zinazoibuliwa na jukwaa hilo kuwa ni ujenzi wa stendi, benki, vituo vya mafuta, masoko, uwekezaji katika usafirishaji na viwanda vya kusindika mazao.

“Kupitia jukwaa hili wilaya itafaidika kwani ina fursa nyingi lakini zilikuwa hazijulikani. Natoa rai serikali iwaongezee bajeti TSN ili kuonyesha fursa zaidi za kiuchumi maeneo mengi nchini,” alisema.

Aliomba halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya kuwekeza kwenye taasisi hiyo ya magazeti ya serikali ili ifanye kazi kwa upeo mkubwa. Alitoa mfano kwa sasa upo utaratibu unaozitaka wizara kutenga bajeti yake kidogo kwa ugonjwa wa Ukimwi, lakini wizara zinaweza pia kutenga bajeti kidogo kwa ajili ya kuiwezesha TSN kufanyakazi yake kwa weledi zaidi,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuhamasisha wawekezaji kwenda Uyui kuwekeza kwani Uyui ina tabia nchi zote za mkoa wa Tabora, kwa sababu inapakana na wilaya zote za mkoa wa Tabora.

“Jiografia yake ni rafiki na ni kitovu cha mkoa kwani huwezi kwenda wilaya yoyote mkoani Tabora bila kupita wilaya ya Uyui. Kwa maana hiyo Uyui ni wilaya ya kimkakati,” alisisitiza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Pima alisema TSN imeuletea mkoa wa Tabora kitu kikubwa kwa kuwa wamefunguliwa milango ya kutangaza fursa lukuki za kibiashara na uwekezaji huko.

“Hii ni faida kwetu, Kaliua sisi tuna fursa nyingi, huu ndio mkoa wa kilimo cha tumbaku, tunalima mpunga kwa wingi, asali, tuna vivutio vya kiutalii visivyopatikana popote nchini, tunalima maharage, karanga, mahindi,” alisema.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Tabora

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi