loader
Picha

Polisi watakiwa kukamata wanaokeketa watoto

JESHI la Polisi mkoani Mara limetakiwa kuwakamata na kuwafi kisha mahakamani watu wanaowakeketa watoto wa kike na kisha kuwaozesha kwa nguvu ili kupata ng’ombe ambazo zinatolewa kama mahari.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lidya Bupilipili alitoa aligizo hilo alipokuwa akifungua mafunzo ya mapambano dhidi ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia katika mkoa huo hivi karibuni wilayani hapa.

“ Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara na wasaidizi wako kamateni watu hao wote na wafikishwe mahakamani. Na vyombo vingine viwachukulie hatua bila kupindisha sheria”, DC Bupilipili alisema katika hotuba wakati akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Mafunzo hayo yalitolewa na shirika lisilo la kiserikali la Matumaini kwa wasichana na wanawake Tanzania Wilaya ya Butiama kama sehemu ya kupambana na vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia.

Bupilipili alisema serikali ya mkoa wa Mara itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirika hilo katika kulinda wasichana ili waweze kufikia ndoto zao za kielimu. Alilipongeza shirika hilo kwa kuanzisha makazi salama ya kuhifadhi wasichana ambao wanakimbia majumbani kwao inapofika wakati wa ukeketaji na wahanga wengine wa ukatili wa kijinsia Mara.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Rhobi Samweli alisema makazi hayo salama yapo Wilaya za Serengeti na Butiama na wameshaokoa wasichana 190 na sasa kuna wasichana 88 katika makazi hayo salama.

“ Nimeambiwa kuwa kuna wahanga 29 katika nyumba salama ya Butiama na 59 katika nyumba salama ya Mugumu. Huu ni msaada mkubwa sana kwa wasichana wanaokwepa ukeketaji”, alisema Bupilipili.

Aliagiza watendaji wa idara za maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii kuwachukulia hatua kali za kisheria, wazazi au walezi ambao wanakataa kupokea wasichana ambao hukimbilia katika nyumba hizo salama na kutaka kurejea nyumbani mara baada ya msimu wa ukeketaji kumalizika.

Mafunzo hayo yanafanyika mwezi mmoja kabla ya msimu wa ukeketaji kufanyika maeneo ya mkoa huo. Bupilipili alisema serikali Mkoani Mara inafanya kila jitihada kuufanya mkoa huo sehemu salama kwa kila mtu wakiwemo wasichana wa shule na kujua ukeketaji ni kosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. “ Nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila mtu anaishi salama pia hofu”, alisema Bupilipili.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Butiama

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi