loader
Picha

Polisi Pwani yavunja mtandao wa wizi wa TV 'Flat Screen'

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kukamata televisheni 10 'Flat Screen' za aina mbalimbali zenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 18.8 ambazo ziliibiwa maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha leo Ijumaa, Kamanda wa Polisi mkoani huko, Wankyo Nyigesa amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane wanashikiliwa kwa tuhuma hizo.

Ameongeza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata jenereta mbili, deki mbili, vingamuzi viwili, spika mbili, redio kubwa mbili na madumu 10 ya lita 20 kila moja ambayo yameibiwa kwenye mradi wa reli ya SGR Soga, Kibaha. Kingine walichokutwa nayo watuhumiwa hao ni kiroba cha bangi.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi