loader
Wanawake wanaopendelea 'fast food' hatarini kuchelewa kupata ujauzito

Wanawake wanaopendelea 'fast food' hatarini kuchelewa kupata ujauzito

Wanawake wanaopendelea vyakula vinavyoandaliwa haraka maarufu kwa jina la ‘fast food’ wanatahadharishwa kuwa kwenye hatari ya kuchelewa kupata ujauzito.

Hii imeelezwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Oxford kilichopo Uingereza baada ya kufanya utafiti wa masuala ya uzazi na kutoa ripoti yake siku za hivi karibuni.

Watafiti hawa waliwahoji wanawake takribani 5,600 wa nchi za Australia, New Zealand, Uingereza na Ireland kuhusiana na vyakula wanavyokula mara kwa mara.

Hata hivyo waligundua kuwa wanawake wengi waliokuwa vyakula vya aina hiyo mara nne au zaidi kwa wiki walichelewa kwa takribani zaidi ya mwezi kushika ujauzito ukilinganisha na wale ambao hawakula vyakula hivyo.

Wataalamu wameeleza kuwa ulaji wa lishe bora huboresha afya ya uzazi na kuongeza nafasi ya kupata ujauzito.

Profesa Claire Roberts wa Chuo Kikuu cha Adelaide, Australia ambaye ndiye aliyeongoza utafiti huo, amesema “kula chakula bora ambacho kimsingi kinahusisha matunda na kupunguza vyakula vya mafuta, huongeza uwezo wa kuzaa.” Vyakula vya ‘fast food’ ni kama chipsi mayai, burger, pizza na vinginevyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/04e7cfee4c72ee795e41cc684bd4e458.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Post your comments