loader
Picha

Wasomi EAC wakutana kujadili tafiti na viwanda

WATAALAM kutoka nchi za Afrika Mashariki wamekutana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kujadili masuala ya tafiti zinazohusu maendeleo ya viwanda.

Mhadhiri Mwandamizi chuoni hapo Ambrose Itika ambaye amemwakilisha Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye kwenye ufunguzi wa mkutano huo, ameeleza kuwa mada hiyo ni muhimu hasa wakati huu ambapo taifa limenuia kuingia katika uchumi wa kati.

Itika alisema UDSM ina uzoefu mkubwa katika masuala ya utafiti na mkutano huo ni sehemu mojawapo ya shughuli za kitaaluma zinazoleta manufaa kwa jamii. “Kuna suala la ushirikiano katika nchi za Afrika Mashariki kwenye sera zinazosaidia maendeleo ya viwanda, ushirikiano wa serikali na sekta binafsi,” alisema.

Naye Profesa Issack Mbecha alisema kama bara nchi zinapaswa kuwa pamoja na kufanya biashara kwa pamoja. Alisema pamoja na uwepo wa rasilimali nyingi katika nchi za Afrika bado ni maskini hivyo zikiungana pamoja zitafanikiwa.

Kwa upande wake Ulingeta Mbamba kutoka Shule Kuu ya Biashara (UDBS), alisema mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo zinaendana na Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Na Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi