loader
Picha

TCU yafungia Chuo Kikuu, yaamuru wanafunzi wahamishwe

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imekifutia usajili kituo cha mjini Moshi cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi(SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kuhamishwa.

Aidha kimezuia udahili wa wanafunzi wapya na kuamuru kuhamishwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaoendelea na masomo katika jumla ya programu tisa. Pia kimeendelea kusitisha udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika vyuo vikuu viwili na kufanya jumla ya vyuo vikuu vilivyositishiwa udahili kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kufikia 12.

Akizungumzia na waandishi wa habari leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU alitaka hatua hizo zisichukuliwe kama siasa. Itakumbukwa kwamba mwaka 2016, TCU ilifanya ukaguzi maalum wa kuhakiki ubora katika vyuo vya elimu ya juu nchini na baadhi ya vyuo viligundulika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoathiri utoaji wa elimu bora.

Aidha alisema tume iliendelea kuvishauri na kuelekeza vyuo kurekebisha mapungufu hayo kwa nyakati tofauti, sambamba na kufanya kaguzi za kawaida na za kushtukiza katika baadhi ya vyuo vikuu.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi