Mtoto wa umri wa miaka mitano nchini Urusi amepata gari aina ya Mercedes Benz baada ya kushinda shindano la kupiga push-up 3200 kwa wakati mmoja.
Mtoto huyo Rakhim Kurayev ambaye pia anafahamika kwa jina la 'Schwarzenegger wa miaka mitano' alipiga push-up hizo kwa muda wa saa 2 na dakika 22.
Kurayev anaripotiwa kuvunja rekodi sita za dunia za mchezo huo kwa nyakati tofauti.
Amepewa gari hilo pamoja na mafasi ya kwenda duka lolote la ma-toy ya watoto na kuchukua chochote anachotaka.
Mmoja wa majaji wa shindano hilo Ramzan Kadyrov ameeleza kuwa Kurayev alifanya push-up 1000 kwa muda wa dakika 40 na sekunde 57, push-up 2000 kwa saa moja na sekunde 47 Pia alifanya nyingine 1419 kwa saa moja, huku 2559 akizifanya kwa saa mbili.