loader
Mwanamke aomba talaka apate watoto wengi

Mwanamke aomba talaka apate watoto wengi

Mahakama Kuu nchini Kenya imekataa kuidhinisha talaka iliyoombwa na wanandoa kwa maelezo kwamba, sababu ya kuomba talaka haina mashiko.

Inadaiwa kuwa, mke alifungua kesi mahakamani kuomba ndoa yao ivunjwe kwa kuwa mumewe amekataa kuzaa watoto wengi.

Wanandoa hao wameishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 8 na wana mtoto mmoja, mwanamke anataka waongeze watoto wengine lakini mumewe anakataa.

Mahakama imeeleza kuwa sababu aliyotoa mwanamke huyo ni ndogo hivyo haiwezi kuidhinisha ndoa hiyo ivunjwe.

Jaji wa Mahakama hiyo George Dulu amewataka wanandoa hao kwenda kutatua mgogoro wao kifamilia kwa kuwahusisha viongozi wa dini hasa ikizingatiwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa Kiislamu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f515ee58a09d8c0c145845adb65becfa.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi