loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wabunge wavuna medali saba Afrika Mashariki

TIMU ya Bunge, Bunge Sports Club, imepata medali saba za dhahabu, kati ya hizo tatu zikiwa zimeletwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Yosepher Komba.

Akizungumza jana, kiongozi wa msafara wa timu hiyo baada ya kushuka kwenye Bombardier 5H-TCE iliyorejea kutoka kwenye Mashindano ya Michezo ya Wabunge wa Nchi za Afrika Mashariki jijini Bujumbura, Burundi, Dk Tulia Ackson alisema mbunge huyo ameipatia timu hiyo medali hizo.

Komba ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chadema, amepata dhahabu katika kukimbia mbio za mita 1,500, 800 na 400. “Katika mbio za kupokezana vijiti pia ameipatia timu hiyo kwa kukimbia kwa kupokezana na wabunge wengine, Rose Tweve, Halima na Zubeda Sakuru katika riadha ya kupokezana vijiti,” alisema Naibu Spika.

Alisema medali ya dhahabu nyingine imeletwa na Naibu Spika, Dk Tulia alipoibuka bingwa wa kwenda mwendo kasi katika urefu wa mita 1,000 na hivyo kuendeleza ushindi huo ambao pia aliupata mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Dk Tulia alisema pia medali nyingine ya dhahabu imepatikana kutoka kwa wabunge wavutaji kamba, lakini pia mchezo wa mwendo kasi kwa wanaume ulifutwa baada wa wachezaji wa nchi nyingine kuleta fujo, na hivyo medali za Tanzania zikapungua.

Alisema medali tano za fedha na shaba zimepatikana katika michezo mingine iliyobaki ikiwemo mpira wa mikono, wavu, kikapu, na riadha kwa wanawake na wanaume. Akizungumza mlezi wa timu hiyo, Mama Salma Kikwete alisema timu hiyo iliondoka Desemba mosi mwaka huu kwenda Bujumbura, Burundi ambako walicheza kwa kujiamini na kufanya vizuri katika mashindano hayo. Alisema ushindi waliopata wachezaji kutoka Tanzania umepatikana kutokana na juhudi walizoonesha katika mashindano hayo na hawakutaka kumwangusha spika wa bunge.

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi