loader
Moyo uliosahaulika ndani ya ndege waibua taharuki Marekani

Moyo uliosahaulika ndani ya ndege waibua taharuki Marekani

Moyo wa binadamu uliokuwa umepakiwa kwenye ndege kutoka uwanja wa ndege wa Seattle, Washington nchini Marekani, kwenda Dallas Texas umesababisha ndege hiyo kugeuza na kurudi uwanja huo wa ndege.

Inaelezwa kuwa moyo huo ambao ulitakiwa kutumika kwa ajili ya upandikizaji, ulisahaulika ndani ya ndege hiyo, ilhali ulitakiwa utolewe na kukabidhiwa kwa aliyetakiwa kukabidhiwa kiungo hicho katika uwanja wa ndege wa Seattle.

Hata hivyo Daktari Bingwa wa Mifupi wa New Orleans Dkt. Andrew Gottschalk alieleza kuwa inawezekana moyo huo kutofaa tena kwa matumuzi yaliyokusudiwa baada ya saa 48, hivyo haikuwa na uharaka sana kwa ndege hiyo kugeuza ili kukabidhi kiungo hicho.

Alieleza pia kuwa abiria hawakuwa na tatizo, ndege yao kugeuza ili tu kuukabidh moyo huo kwa wahusika.

“Abiria waliingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa moyo huo ulihitajika kwa ajili ya upandikizwaji hivyo, na hivyo uamuzi wa rubani kugeuza ndege, uliafikiwa, ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni kuokoa maisha ya mtu,” aliongeza. 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a9a451adb4d2c71d1511e574df79a2ea.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi