loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Matola aipa neno Simba

KOCHA wa Lipuli FC, Suleiman Matola amesema kucheza kwa kujituma na kutanguliza malengo ni mbinu itakayokisaidia kikosi cha Simba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao kimataifa dhidi ya Nkana FC ya Zambia na kutinga hatua ya makundi.

Mchezo huo wa raundi ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika, unatarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja wa taifa wa Dar es Salaam, baada ya ule wa awali uliopigwa Kitwe, Zambia wenyeji Nkana kupata ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza na gazeti hili jana Matola, alisema bingwa huyo mtetezi wa Ligi Kuu ana kikosi kizuri na kipana na kwamba kinachotakiwa kwa wachezaji wake ni kufuata maelekezo ya kocha wao na kucheza kwa nidhamu ili kupata ushindi. “Wachezaji wa Simba wanatakiwa kujiandaa vizuri, wasibweteke na bao walilolipata ugenini, Nkana ni timu nzuri,hata wachezaji wa Simba ni wazuri pia kinachotakiwa kocha wa Simba Patrick Aussems kuhakikisha anatengeneza muunganiko mzuri wanaweza wakapata mabao mengi,”alisema Matola aliyewahi kuwa mchezaji wa kikosi hicho na hatimaye kocha msaidizi.

Alisema wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanawazuia washambulia wa wapinzani wao wasipate nafasi ya kufunga bao na kuhakikisha wanatumia vyema nafasi watakazozipata ili kuhakikisha katika kipindi cha kwanza wanapata bao la mapema ili kuwachanganya wapinzani hao kama walivyofanya kwa Mbabane Swallows, eSwatini walioshinda jumla ya mabao 8-1.

Katika mchezo huo wa kesho timu itakayoibuka na ushindi katika itafuzu hatua ya makundi. Ushindi wa bao 1-0 utaivusha Simba na kurudia historia ya mwaka 2003 ilipotinha hatua ya makundi kwa kuifunga Zamalek ya Misri. Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’ Abraham Morice (kulia) akichezesha droo ya fainali za AFCON U-17 katika hafla iliyofanyika juzi Mlimani City, Dar es Salaam.

Kushoto ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Adolf Rishard. (Picha na Rahel Pallangyo) JUVENTUS, Italia CRISTIANO Ronaldo anatarajiwa kucheza dhidi ya Roma leo kabla ya kupumzishwa katika moja ya mechi mbili za ‘fainali’ kwa mwaka 2018, Massimiliano Allegri alithibitisha. Bosi huyo wa Juve aliahidi nkumpa nyota huyo wa Ureno angalau mechi moja Desemba huku Ronaldo akicheza dakika 90 kwenye mechi zote za Serie A isipokuwa moja msimu huu.

Allegri anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kucheza dhidi ya Roma, wakati Juve ikiwania kuendeleza rekodi yake ya kutokufungwa katika kutetea taji lao, lakini anafuraha kuona Ronaldo akikosa safari ya kwenda Atalanta kwenye ‘Boxing Day’ au kwenye mechi dhidi ya Sampdoria Desemba 29. “Ronaldo atacheza kesho (leo), kisha atakosekana katika mechi mbili zijazo,” alisema Allegri kwneye mkutano na waandishi wa habari jana.

Mechi ya leo katika uwanja wa Allianz Juve inakutana na Roma iliyocheza mechi tano mfululizo bila ushindi kwenye michuano yote kabla ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Genoa Jumapili iliyopita. Presha iko kubwa kwa kocha mkuu Eusebio Di Francesco, lakini Allegri alisisitiza ushindi. “Ni timu nzuri, pamoja na mambo mengine, ni timu pekee ya Italia pamoja na Juventus bado zipo kwenye Ligi ya Mabingwa,” alisema.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi