Wachimba migodi 15 waokolewa Zimbabwe

KIKOSI cha waokoaji jana Jumapili kimewaokoa wachimbaji wote 15 wa mgodi wa kujikimu walionasa chini ya shimo katika mgodi wa Redwing nchini Zimbabwe baada ya kuporomoka siku ya Alhamisi, msemaji wa serikali alisema.

Wachimba migodi hao walinaswa baada ya ardhi kuporomoka kwenye mgodi huo, kilomita 270 Mashariki mwa mji mkuu Harare.

“Wachimba migodi wote waliokolewa wakiwa hai,” msemaji wa serikali Nick Mangwana aliongeza.

Shughuli ya uokoaji ilikuwa imechelewa kutokana na ardhi kutokuwa rafiki kulingana na kampuni ya Metallon Gold, inayomiliki Redwing.

Habari Zifananazo

Back to top button