loader
Trump, Kim Jong Un kukutana hivi karibuni

Trump, Kim Jong Un kukutana hivi karibuni

RAIS wa Marekani, Donald Trump amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Korea Kaskazini (DPRK), Kim Jong Un ambayo pamoja na mambo mengine imeelezwa kuwa viongozi hao wanatarajia kukutana hivi karibuni kwa mkutano wao wa pili.

Trump aliwathibitishia waandishi wa habari Ikulu ya Marekani kuwa ni kweli amepokea barua hiyo kutoka kwa Kim. “Tunatarajia kuwa na mkutano mwingine… tutapanga kuhusu kufanyika kwa mkutano huo muda mfupi ujao,” alieleza Trump. Kauli hiyo ya Rais Trump imekuja siku moja baada ya Pyongyang kuonesha dalili kuhusu kutaka kusitisha mpango wake wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Imeelezwa pia kuwa katika hotuba yake ya Mwaka Mpya Jumanne wiki hii, Kim alisema angependa kuharakisha mpango huo wa kusitishwa kwa silaha za nyuklia na alikuwa tayari kukutana na Trump wakati wowote. Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pia alisisitiza nia yake ya kutaka kujenga mahusiano mapya na Washington kwa masharti kwamba Marekani nayo inapaswa kuchukua hatua kama hizo.

Imeelezwa kuwa mahusiano kati ya DPRK na Marekani yalianza kuimarika mwaka jana na mkutano wa kwanza kati ya Trump na Kim ulifanyika nchini Singapore mwezi Juni mwaka jana. Kwa sasa, tofauti kati ya mataifa hayo mawili zimebaki kwenye mambo ya msingi kama vile usitishwaji wa silaha ya nyuklia, vikwazo vya Marekani pamoja na kutolewa kwa tamko la kumalizika kwa vita.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/25a24136e7755f52c5703d3629e8c7f0.jpeg

KAMPUNI ya Qnet imezindua ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi