loader
Picha

Jaribio la kupindua serikali Gabon lakwama, wanajeshi washikiliwa

Serikali ya Gabon imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi baada ya wananjeshi kadhaa kuvamia kituo cha redio cha taifa na kutangaza kuwa Rais Ali Bongo amepinduliwa.

Rais Bongo yupo nchini Morocco kwa mwezi wa pili sasa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kiharusi.

Hata hivyo wanajeshi waliohusika na tukio hilo wanashikiliwa , gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti.

Msemaji wa serikali hiyo, Guy-Bertrand Mapangou ameripotiwa akisema kuwa tayari kituo hicho cha utangazaji kimesharejeswa chini ya usimamizi wa serikali hivyo mambo sasa yanakwenda shwari.

Mapema leo Jumatatu, mtu aliyejitambulisha kama Lt Kelly Ondo Obiang akiwa na walinzi waliovalia mavazi kama ya walinzi wa Rais wa Taifa hilo walitangaza kupitia kituo hicho cha redio kuwa wametwaa madaraka na kila mwananchi asalimu amri.

SERIKALI ya Uganda imeahirisha kufungua shule kwa mwezi mmoja zaidi ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi