loader
Picha

Mpinzani Felix Tshisekedi atangazwa mshindi urais DRC

Kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi, ameshinda uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tume ya Uchaguzi (CENI) yatangaza kuamkia leo.

Matokeo yaliyochapishwa na BBC yanaonesha kuwa, kati ya wapigakura asilimia 48 waliojitokeza, Tshisekedi amepata jumla ya kura 7,000,000, akifuatiwa na Martin Fayulu aliyepata kura 6,400,000 huku Emmanuel Shadary akiambulia kura 4,400,000.

Endapo akithibitishwa, Tshisekedi anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka upinzani kushinda urais wa DRC, tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1960.

Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya kudumu kwa miaka 18, akipokea kiti hicho kutoka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuawa kwa risasi.

SERIKALI ya Uganda imeahirisha kufungua shule kwa mwezi mmoja zaidi ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi