loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Venezuela yavunja uhusiano na Marekani

RAIS wa Venezuela, Nicolas Maduro, ameishutumu Marekani kwa kuandaa mapinduzi katika taifa hilo la Amerika ya Kusini, hivyo imetangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na nchi hiyo.

Katika hotuba yake ya jana, Maduro amewaamuru wanadiplomasia wa Marekani kuondoka nchini humo kwa kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi. Maduro alimtaka Rais wa Marekani, Donald Trump, kuacha kuifuatilia Venezuela. Alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wanadiplomasia wa Venezuela waliorudishwa nchini humo kutoka Marekani na kumweleza Rais Trump “Weka mikono yako mbali na Venezuela.”

“Trump, wewe unahusika na vurugu yoyote itakayotokea Venezuela…damu itakayomwagika Venezuela iko mikononi mwako, Rais Donald Trump,” alisema. Maduro ambaye ni rais aliyechaguliwa kidemokrasia mara mbili, amemwita kiongozi wa upinzani, Juan Guaido kama kibaraka wa Marekani pamoja na kuishutumu Marekani kwa jaribio la kuandaa mapinduzi nchini humo.

Wakati huohuo, Utawala wa Trump umeiwekea vikwazo kampuni ya mafuta inayomilikiwa na Serikali ya Venezuela, kama sehemu ya kumshinikiza Rais Maduro ajiuzulu na kuachia madaraka kwa kiongozi wa upinzani Guaido anayeungwa mkono na Marekani. Sintofahamu hiyo nchini Venezuela imetokana na viongozi hao wawili, yaani Rais Maduro na kiongozi wa upinzani, Guaido kila mmoja kudai kuwa ni mshindi halali wa urais katika uchaguzi uliofanyika Mei mwaka jana.

Tangu Januari 15 mwaka huu, hali ya usalama nchini humo imeendelea kuwa tete hasa pale bunge ambalo kwa sehemu kubwa linadhibitiwa na upinzani kutangaza kuwa Maduro amepora madaraka. Kiongozi wa upinzani, Guaido alijitangazia Januari 23 mwaka huu kuwa rais wa mpito na kuifanya Marekani na nchi zingine kumtambua kama kiongozi wa nchi. Aidha, kiongozi huyo wa upinzani alivieleza vyombo vya habari kuwa alikuwa na mazungumzo na Rais Trump kujadili hali ya kibinadamu nchini Venezuela. “Ndiyo, nimezungumza na Rais Trump pamoja na marais wengine katika ukanda huu. Mazungumzo yetu yalijikita kuhusu watu na hali ya kibinadamu nchini Venezuela,”alieleza Guaido.

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: CARACAS, Venezuela

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi