loader
Simba kuanza na Mwadui

Simba kuanza na Mwadui

MSHIKEMSHIKE wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea tena leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa kuwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba SC dhidi ya Mwadui FC.

Simba itamalizia hasira zake kwa Mwadui baada ya kufungwa 5-0 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika uliofanyika Alexandria, Misri wiki iliyopita.

Kabla ya mechi za jana, Simba ilikuwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33 Mwadui ikiwa nafasi ya 16 na pointi zao 24.

Simba itahitaji kupata ushindi leo kwa udi na uvumba ili kujipoza na kipigo walichokipata Jumamosi iliyopita cha mabao 5-0 kutoka Al Aly na pia kujiwekea mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wao.

Mwadui wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya, kwani mara ya mwisho timu hizi zilipokutana Septemba 23 mwaka jana, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1, mabao ya Simba yakifungwa na John Bocco aliyepiga mawili na jingine Meddie Kagere.

Nahodha wa Simba, Bocco amesema, mashabiki wa timu yao watulie na wasiwe na wasiwasi kwani matokeo mabaya waliyoyapata katika mechi iliyopita ya klabu bingwa hayatawaathiri katika mechi zao za ligi.

“Tumetoka katika michezo ya kimataifa, tumeshamaliza na mechi iliyopita tupo tayari na mchezo wa ligi ili tufanye vizuri,” alisema Bocco.

Kwa upande wa Mwadui katibu wa timu hiyo, Ramadhani Kilao alisema kuwa wao wamejiandaa kwa lolote kuweza kuwakabili Simba na wamepanga kuondoka na pointi katika mchezo huo.

“Kikosi chetu kipo hapa Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo tunachokiangalia ni kupata pointi tatu ili kujitengenezea mazingira ya kujiweka sehemu salama ya msimamo wa ligi,” amesema Kilao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8f6ec5d13015eb2b9d8ef54de22f5f47.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi