loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nkamia aponda makocha

MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema ni aibu Tanzania kuchukua makocha kutoka nje huku kukiwa na wazawa wenye uwezo mkubwa.

Akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2018-2019, Nkamia alisema ni aibu kwa kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi. “Ni aibu kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi huku wazawa wakiwa hawapewi nafasi,” alisema.

Nkamia aliyewahi kuwa kiongozi kwenye klabu ya Simba miaka ya nyuma alisema pia kwa sasa Ligi ya Soka ya Wanawake na Ligi Kuu imekuwa mahututi kutokana na timu kulia njaa. “Hata Ligi ya Wanawake hali sio nzuri, mfano timu inatoka nyumbani na ugenini timu inatoka Njombe haina hata sehemu ya kulala kwa sababu ya ukata, hatuwezi kuendesha mpira hivyo.”

Kutokana na kauli hiyo, Spika Job Ndugai alisema: “Mheshimiwa Nkamia, sio timu za kina dada tu hata timu fulani zinatembeza bakuli mheshimiwa Nkamia.” Katika hatua nyingine, Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (CUF) amehoji ni kiasi gani cha fedha ambacho kimekuwa kinatolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).

Akiuliza swali jana bungeni, Haji alihoji: “FIFA inatoa misaada ya fedha kwa kupitia TFF. Je, ni kiasi gani cha fedha TFF imekuwa ikiipatia Zanzibar kupitia ZFA?” Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alisema ni kweli FIFA inatoa msaada wa fedha kwa mashirikisho ya mpira wa miguu ikiwemo TFF kwa ajili ya miradi na programu mbalimbali.

Alisema fedha hizo huwa ni maelekezo maalum kwa lengo la kusaidia na kuendeleza maeneo ya Ligi ya Wanawake, Vijana pamoja na masuala ya kiutawala. “Kuanzia mwaka huu FIFA itakuwa inatoa jumla ya dola za Marekani milioni 1.25 kila mwaka kwa wanachama wake ikiwemo ZFA ambayo ni sehemu ya TFF,”alisema. Akifafanua mchanganuo wa fedha hizo, Shonza alisema fedha za miradi kiasi cha dola za Marekani 750,000, fedha kwa ajili ya kuendesha ofisi dola za Marekani 500,000.

“Hata hivyo kwa muda wa miaka mitatu kutokana na kutokuwepo kwa uwazi katika matumizi ya fedha na kukidhi vigezo vya utawala bora, TFF wamekuwa hawapati hizo fedha,” alisema Shonza. Shonza alisema kazi kubwa imefanyika kurekebisha dosari zilizokuwepo za kiuhasibu na utawala bora hivyo uwezekano ni mkubwa TFF na ZFA kuanza kupokea msaada huo wa fedha mapema mwaka huu.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi