loader
Wawekezaji katika elimu watakiwa kuchangamkia fursa Lindi

Wawekezaji katika elimu watakiwa kuchangamkia fursa Lindi

WAWEKEZAJI katika sekta ya elimu ndani na nje ya nchi wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika sekta hiyo mkoani Lindi kwani hadi sasa mkoa huo haujafanya vizuri katika eneo hilo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati wa kikao cha maandalizi ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Lindi linalotarajiwa kufanyika Machi 25 hadi 27, mwaka huu.

Kwa mujibu wa DC huyo, mpaka sasa bado Lindi haijafanya vizuri katika uwekezaji wa elimu kiasi cha takribani asilimia 95 ya watumishi wa mkoa huo kupeleka watoto wao katika shule za mikoa ya jirani. Ndemanga alisema kupitia jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji, wamejipanga kuvutia wawekezaji katika elimu ili mkoa huo uwe na shule za kisasa na vyuo vya elimu ya juu kama ilivyo mikoa mingine.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema hadi sasa pamoja na kuwepo kwa shule za serikali, hali haiko vizuri kwa upande wa shule binafsi na hata zilizopo baadhi hazina rekodi nzuri ya ufaulu.

“Kati ya mambo tunayoyapa kipaumbele ni uwekezaji katika eneo hili la biashara, hii ni fursa kubwa. Tunaomba wafanyabiashara na wawekezaji waichangamkie,” alisisitiza Zambi alipozungumzia jukwaa.

Alisema baadhi ya vyuo vimeomba maeneo yavujenzi wa kampasi zake kikiwemo Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM). “Ninatarajia baada ya jukwaa hili, tutabaki na neema kwa upande wa elimu pia. Natarajia tutapata mwamko mzuri wa kuhakikisha kiwango cha elimu Lindi kinatoka hapa kilipo na kupanda,” alisisitiza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fde9d068671730ae6f56b3a426500885.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Lindi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi