loader
Watoto 1900 Dar wapata baba

Watoto 1900 Dar wapata baba

UKIWA umepita takribani mwaka tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda uwaite wanawake waliotelekezwa wakiwa na mimba au watoto, zaidi ya watoto 1900 wamepata baba zao na wanatunzwa.

Makonda ameyasema hayo leo mchana alipohudhuria maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani, kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Amesema, wanaume wengi wamejitokeza na kuanza kutunza watoto wao ambao awali waliwatelekeza.

“Zoezi hili limekuwa la mafanikio makubwa, na wanaume wengine waliamua kukutana na wanawake waliowatelekeza, na kuyamaliza chinichini ili kuepukana na aibu,” amesema Makonda.

Makonda amewaeleza wanawake kuwa ni lazima wafahamu kwamba, pindi tu mwanamke anapopata ujauzito, baba wa mtoto anawajibika kuanzia siku ujauzito huo unapogundulika, na si baada ya mtoto kuzaliwa.

Amesema, aliandaa timu ambayo imefanya uchambuzi wa mapungufu ya sheria kuhusiana na wanaume kuhusika kwenye malezi ya watoto tangu mwanamke anapopata ujauzito.

“Tayari wanashapata mapungufu hayo na tumeyaweka kwenye ripoti maalumu ya mapendekezo ambayo nitaikabidhi kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ili ayawasilishe bungeni kwaajili ya kufanyiwa mabadiliko ya sheria, “ amesema Makonda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/97810d5765ec8fa4bec6fb2e2970df61.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi