loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rwanda wapania mashindano ya baiskeli ya Afrika

TIMU ya taifa ya waendesha baiskeli ya Rwanda iko katika maandalizi makali kwa ajili ya mashindano ya Afrika yaliyopangwa kufanyika katika mji wa Bahir Dar, Ethiopia, imeelezwa.

Hayo ni mashindano ya 14 ya kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005. Wapanda baiskeli bora Afrika wiki hii watakuwa njiani kuelekea katika mashindano hayo makubwa yatakayoshirikisha timu za taifa.

Rwanda ilikuwa mwenyeji wa mashindano kama hayo mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari juzi, kocha wa timu ya vijana ya (wanaume na wanawake) na ile ya wanawake ya wakubwa, Nathan Byukusenge alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanaangalia mbele kwa wapanda baiskeli wao kufanya vizuri Ethiopia.

“Maandalizi yetu yanaendelea vizuri, na wachezaji wetu wako vizuri tayari kwa mashindano hayo ya Addis Ababa, tuko tayari kukabiliana na wapanda baiskeli bora Afrika, tunajiamini na uwezo wetu,” alisema Byukusenge, ambaye aliwakilisha nchi katika mashindano ya Mountain Bike katika Olimpiki ya 2016 Rio, Brazil.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi