loader
Makonda kumsaidia kijana aliyevunjika mguu

Makonda kumsaidia kijana aliyevunjika mguu

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kumsaidia matibabu kijana, Hamis Hashimu baada ya mwaka 2013 kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na aliporejea, hali iliendelea kuwa mbaya zaidi ya ilivyokuwa awali.

Hamis (16) anasumbuliwa na ugonjwa wa mguu kujaa maji na kuvimba kupita kiasi tatizo ambalo limemuanza tangu mwaka 2008. Makonda amechukua jukumu la kumtibu kijana huyo baada ya kubaini anaishi katika mazingira magumu katika chumba cha kupanga Yombo Dovya jijini Dar es Salaam huku akiishi kwa kuomba omba mtaani ili apate mlo.

Katika kuhakikisha anapitwa matibabu na kurejesha ndoto zake, Makonda jana alifanikisha Hamis kufikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Dharura (MNH), Dk Juma Mfinanga.

Akizungumza Dk Mfinanga alisema: “Kwa sasa tumempokea na taratibu za kumuandikisha ustawi wa jamii zinafanyika ili aweze kupelekwa wodini na kuanza matibabu. “Uchunguzi zaidi utafanyika kuangalia na namna gani tutaweza kuokoa maisha yake na kumrejesha kwenye hali yake ya kawaida, uwezekano wa kupona upo ila Watanzania muwekeni kwenye maombi, sisi kama madaktari tutatekeleza wajibu kwa kadri ya uwezo wetu, mengine ni kudra za Mwenyezi Mungu.”

Naye Makonda, alisema: “Nitamsaidia Hamis gharama zote za matibabu mpaka pale atakapopona, kuna watu wanamtumia kama kitega uchumi, kuanzia sasa nitadili nao, Watanzania wasidanganyike na matapeli maana kuna wimbi la watu wanasambaza meseji kwenye mitandao ya kijamii tumsaidie Hamis tuma namba hii, hicho kitu hakipo.” “Nasema yeyote atakayemgeuza Hamis kitega uchumi nitadili naye,” alisisitiza Makonda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3c0519b246f1f4734518f3e25eaf6b97.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi