loader
Majaliwa kuongoza shangwe Taifa Stars

Majaliwa kuongoza shangwe Taifa Stars

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo kati ya timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars na Uganda, The Cranes.

Mchezo huo wa mwisho wa kukata tiketi ya kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika ‘Afcon’ zitakazofanyika Misri Juni mwaka huu, unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam keshokutwa jioni. Mwenyekiti wa kamati ya kuhamasisha ushindi kwa timu za taifa, Paul Makonda aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, lengo ni kuonesha serikali inaungana na Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa ari wachezaji.

Kamati hiyo ilikutana jana kwa mara ya pili ambapo walijitokeza wasanii mbalimbali na watu maarufu nchini wakiwa na nia ya kuongeza hamasa kwa Watanzania wote kutokana na ushawishi wao. “Tunafahamu umuhimu wa mchezo huu Watanzania wote ni nafasi yetu ya mwisho kama tutafanikiwa kushinda, basi tutakata tiketi kwenda kushiriki fainali safari hii nchini Misri, Waziri Mkuu kama mdau wa soka atakuwa nasi pamoja kushangilia timu yetu,” alisema Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Makonda amewapongeza watu wote mashuhuri waliojitolea kuwanunulia watanzania tiketi kwenda kuangalia mchezo huo akiwemo Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga aliyenunua tiketi 100. Aidha Makonda kuonesha msisitizo kwenye jambo hilo amenunua tiketi 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu kutumia fursa hiyo kwenda kuishangilia timu kwa pamoja. Mbali na hilo, Makonda pia ameagiza daladala zote kuelekeza ruti ya kupeleka mashabiki Uwanja wa Taifa. “Kama gari linafanya safari zake kutoka Bunju, Tegeta lichukue abiria kwenda Uwanja wa Taifa.” Naye Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo alisema maandalizi ya kikosi hicho yanaenda vizuri na kwa siku wanafanya mazoezi mara mbili.

“Kwa siku wanafanya mazoezi mara mbili, asubuhi wanafanya Uwanja wa Boko na jioni wanafanya Uwanja wa Taifa, hiyo yote ni kuhakikisha tunajiandaa vizuri kwenye mchezo dhidi ya Uganda kupata matokeo,” alisema Ndimbo. Ndimbo alisema kwa kujali umuhimu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo wamepunguza kiingilio na kuweka bei ya chini ili kuwapa fursa watu wote kujitokeza uwanjani siku hiyo. “Kwa viti vya mzunguko Sh 2,000, VIP B, C Sh 10,000, kwa viti vya VIP A Sh 20, 000 na kutakuwa na tiketi za platinum bei yake ni Sh 100,000 gari unaenda kupaki Serena na unasafirishwa na gari moja kwenda Uwanja wa Taifa,” alisema Ndimbo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d29f5abbb85896feb6edd1e1165888ea.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi