loader
Kila mchezaji Taifa Stars kupewa mil. 10/-

Kila mchezaji Taifa Stars kupewa mil. 10/-

MWENYEKITI wa kamati ya hamasa kwa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Paul Makonda amesema ahadi ya kupewa sh milion 10 kwa kila mchezaji imeanza kufanyiwa kazi na kila mmoja atapata fedha zake kama walivyoahidiwa.

Kabya ya machi kati ya Taifa Stars na timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' Makonda aliahidi kwamba, endapo wangeshinda kila mchezaji wa Taifa Stars angepewa Sh milioni 10.

Taifa Stars waliinyuka The Cranes mabao 3-0 hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika ‘Afcon 2019. Makonda amewashukuru Watanzania waliojitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa jana, Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema alipopewa jukumu hilo awali na Shirikisho la soka Tanzania (TFF), alijua anakibarua kigumu akaomba ruhusa kumteua kwenye kamati hiyo Haji Manara (msemaji wa Simba) na Jerry Muro (Mkuu wa Wilaya ya Arumeru) kwa sababu wawili hao wanatoka kwenye klabu kubwa za Simba na Yanga na zinawafuasi wengi jambo ambalo wamefanikiwa .

“Nawashukuru wanakamati wote kwa kufanya kazi nzuri tuliyopewa na TFF, kwanza kuhakikisha timu inashinda, pili kurudisha timu kwa watanzania jambo ambalo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa watu walishikamana pamoja bila kujali itikadi zao klabu zao na kutanguliza umoja wa taifa kwanza,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alitoa Sh milioni moja kwa Ikuzi Kicheko ‘Mzalendo’ aliyetoka Manyara kuja Dar es Salaam na kupita mitaani kuhamasisha watanzania kwenda uwanjani.

Makonda alisema kwa kuthamini makundi yote aliyofanya nao kazi kwa pamoja na kufanikiwa kwa asilimia 100 kutimiza majukumu waliyopewa, keshokutwa kunatarajiwa kufanyika hafla kubwa ya kihistoria ambayo haijawai kutokea nchini kuwapongeza kwa kazi waliyofanya.

Alisema kwenye hafla hiyo ambayo itafanyika kwenye Hotel ya Serena meza moja ya vyakula itanunuliwa kwa Sh milioni 10,ambapo hadi sasa kampuni kubwa 50 zimeshathibitisha kushiriki kwenye tukio hilo na kuyaomba mengine yanayohitaji kuunga mkono kujitokeza milango iko wazi.

“Niwaambie tu waandishi wa habari fedha ambazo zitachangishwa kwenye hafla hiyo ya kipekeae zitawekwa kwenye mfuko maalumu kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha timu hiyo kwa michezo ijayo,” alisema.

Makonda alisema anawakumbuka wachezaji wote walioipeleka timu kwenye Afcon mwaka 1980 Lagos, Nigeria na kwamba ujumbe wao umefika kwenye mamlaka husika na unafanyiwa kazi kuhakikisha kila mtu anapata stahiki yake kwa kulifanyia mema taifa hili.

Kauli hiyo ya Makonda imekuja kufuatia malalamiko ya baadhi ya wachezaji wa kikosi kilichokwenda Lagos baada ya mwenzo Peter Tino kupewa sh milioni tano na rais John Magufuli alipokwenda Ikulu na kikosi cha Stars kwa mwaliko wa rais.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9779274632a37869935cc50ac8d7f183.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi