loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pierre Liquid atikisa bungeni

MSANII wa vichekesho, Peter Mollel maarufu Pierre Liquid ametikisa Bunge baada ya kutinga na kushangiliwa na wabunge. Pierre alifika bungeni jana kwa mwaliko wa Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Ditopile (CCM).

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali, Spika Job Ndugai alimtaka Ditopile amtambulishe Pierre kwa kuwa yeye hamfahamu. “Nina mgeni lakini simfahamu naomba nimpe heshima Ditopile atumie dakika moja kumtambulisha maana simfahamu,” alisema Ndugai.

Akimtambulisha Pierre, Mariam alisema ni Mtanzania (huku Pierre akisimama na kujipinda mtindo wake maarufu) mzalendo mjasiriamali wa samani za ndani anayepatikana Chang’ombe ni mpenda burudani na ana kijiwe kinachoitwa Liquid. “Lakini hivi karibuni ametokea kupata umaarufu wa hali ya juu sio kwa nchi yetu hadi nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na sanaa na vichekesho.

“Pierre ni maarufu na kwa kauli zake ambazo huwafurahisha watu na hata kama una msongo wa mawazo anauondoa hakika Mheshimiwa Spika utabaki kuwa kileleni, utakuwa juu. “Lakini mzalendo huyu kutokana na uzalendo ambao ameuonesha kina Mzee Majuto leo tunawaenzi kutokana na usanii, kina Mr Bean ni mabilionea kutokana na kipaji cha vichekesho,” alisema.

Mbunge huyo alisema ni mmoja ya watu waliojitoa mhanga kuleta hamasa katika timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kushinda ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uganda, katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019 Misri. “Napenda kumalizia, Pierre anasadifu maneno ya wahenga wanaosema Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua,” alisema Mariam, huku akishangiliwa.

Spika alimkaribisha Pierre huku akitumia maneno yake ya utabaki juu, utabaki kileleni. Mara baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, Pierre alikutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye aliahidi kumpatia tiketi ya ndege kwenda kuishangilia Stars katika michuano hiyo ya Afcon nchini Misri. Waziri Mkuu alimtaka msanii huyo kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars kwa kuisemea vizuri.

LIGI Kuu Soka ya Wanawake inaendelea leo ikiwakutanisha wakina dada ...

foto
Mwandishi: Maulid Ahmed, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi