loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usajili visima vya maji muhimu kwa afya

MAJI ni suala ambalo linamhusu kila mtu lakini maji haya kama hayatakuwa safi na salama ni hatari katika afya za watumiaji pamoja na kuathiri uchumi wa nchi pamoja na mazingira.

Katika baadhi ya maeneo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na jiji la Dar es Salaam kumekuwa na tatizo la uhaba wa maji unaotokana na utunzaji mbaya wa vyanzo vya rasilimali za maji.

Kutokana na changamoto za uhaba wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali baadhi ya watu wameamua kuchimba visima ili wapate maji.

Hata hivyo katika uchimbaji huo wa visima, inawezekana kuwa changamoto ya maji itakwisha lakini ni kwa muda mfupi huku ikitengenezwa changamoto ya muda mrefu ya kuyapoteza maji kabisa kutokana na uvunaji maji kiholela.

Kama wananchi hawatafuata utaratibu uliowekwa katika uchimbaji wa visima hivi ni hatari. Lakini pia mbali na kuyapoteza maji, watu wanapoamua kuchimba kisima chake kupitia kampuni au mtu binafsi anayemjua bila kuzingatia sheria ni hatari kiafya pia.

Uchimbaji huu holela wa visima unaofanywa na watu usiozingatia matakwa ya kisheria, unaweza kuwa ni uelewa mdogo wa jamii juu ya usimamizi, utunzaji, uboreshaji na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa jamii.

Kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inafanya utambuzi wa wamiliki wa visima na kutoa elimu ya usimamizi na utunzaji wa rasilimali za maji kwa wananchi.

Aidha, Bodi hii inawahimiza wananchi kusajili visima vyao kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na.11 ya mwaka 2009 pamoja na faida nyingine za usajili huo, ni pamoja na kulinda afya za watu na kuboresha mfumo wa takwimu za maji chini ya ardhi ndani ya bonde.

Hii itasaidia wananchi kuwa na uhakika wa kutumia maji safi salalma, kwa kuwa usajili wa visima unakwenda sambamba na upimaji wa ubora wa maji.

Ili kuhakikisha tunakuwa na maji safi na salama ni muhimu kuhakikisha watu wenye visima wanasajili visima vyao.

Uchimbaji na uchukuaji wa maji chini ya ardhi huu holela ni hatari kwa afya kwani kunaweza kusababisha kuvuta maji taka kutoka kwenye vyoo vya mashimo kutokana na umbali kati ya kisima cha maji na shimo la maji taka.

Aidha, hatari nyingine ni mifereji ya maji machafu na kuathiri ubora wa maji chini ya ardhi. Watu wanapochota maji haya, hutumika katika matumizi mbalimbali ya nyumbani kama vile kunywa, kupikia, kuoga na wengine kumwagilia katika bustani za mboga.

Hali hii husababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu kwa watu ambao wanatumia maji haya na pengine wasijue kisababishi ni nini.

Uvunaji huu wa maji chini ya ardhi husababisha pia kukauka kwa visima vya maji hasa vile vifupi baada ya kina cha maji kushuka, hali ambayo imekwishajitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha wananchi kuwa na uhaba wa maji kwa kuwa mchakato wa kuchimba kisima kirefu unagharimu fedha nyingi.

Katika kuhakikisha kuwa vyanzo endelevu vya maji, lazima tuelimishane na hatimaye tushirikishane juu ya dhana nzima ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji, kutokana na ukweli kwamba maji ni uhai na bila maji hakuna maisha.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi