loader
Samia awashangaa wanaohoji ulinzi wa Rais

Samia awashangaa wanaohoji ulinzi wa Rais

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewashangaa wanasiasa wanaohoji ulinzi wa Rais John Magufuli, badala ya kuhoji maendeleo yanayofanywa na serikali.

“Leo wakati nasikiliza dondoo za magazeti kuna mtu alikuwa anahoji ulinzi wa rais. Nikajiuliza anataka kufanya nini? Inaonesha wenzetu hawa kwa maendeleo yaliyopo wameanza kufilisika mawazo na kipi cha kuzungumza ndani ya nchi. Hawawezi kusema maendeleo kwani watakuwa wanajitia kisu cha tumbo,” alisema Samia.

Makamu wa Rais aliongeza, “Watanzania tupo nyuma yako. Tutaungana kwa yale unayotuelekeza. Nchi itajengwa na Watanzania wenyewe.

Sisi tunakupongeza sana.” Juzi akizungumza Bungeni, Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (CCM), amesema suala la ulinzi kwa Rais John Magufuli linahitajika liwe kubwa zaidi kutokana na mambo makubwa anayofanya ya kunyoosha nchi.

Ameyasema hayo bungeni jana wakati akichangia kwenye mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ambao alitumia nafasi hiyo kumjibu Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema).

Mbowe wakati akichangia elieleza kuwa amekutana na msafara wa Rais, lakini ameogopa kwa alichoeleza kuwa anasindikizwa na magari zaidi ya 80.

Akichangia suala hilo, Kingu alisema “Suala la ulinzi na usalama kwa Rais lazima liwe kubwa..nashauri ulinzi wa Raia uongezwe maradufu maana hatuwezi kuacha kutokana na mambo makubwa anayofanya hivyo usalama wake haupo sawa.

” Kingu alifafanua kuwa kwenye suala la utawala bora hakuna mahali palipoandikwa kuwa chama fulani kifanye vurugu au kundi la watu fulani.

“Jimbo ninalotoka Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) wameletewa kiasi cha shilingi bilioni 1.3, tuna madaraja na vituo vya afya hayo ni mambo ya utawala bora tunayohitaji,” alieleza.

Alifafanua kuwa hata kwenye Jimbo la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), serikali imepeleka maji katika vijiji vingi na watu wanafaidika na huduma hiyo licha ya kuwa hayupo.

“Msije hapa kuudanganya umma kwamba CCM chini ya Rais John Magufuli inafanya kazi kubwa na 2020 anachukua kura zaidi ya asilimia 95,” alisema.

Wakati Kingu akizungumza Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) aliomba utaratibu kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya Bunge namba 64 ambapo aliruhusiwa kuzungumza.

“Mheshimiwa Mwenyekiti tupo hapa kudhibiti matumizi ya fedha anachozungumzia Mbunge Kingu inaonesha kama Bunge tumepewa fadhila na serikali wakati tumekuja kusimamia kodi za wananchi,” alisema Msigwa Baada ya Msigwa kumaliza kuzungumza Mwenyekiti wa kikao hicho, Andrew Chenge alimtania Msigwa kwamba alikuwa na nia ya kuchangia tu.

“Lakini Kingu anatukumbusha sisi kama wabunge yanayofanywa na serikali kupitia bajeti bila kujali unatoka chama gani au ni mbunge gani maana serikali inasukuma maendeleo na ndio hoja yake,” alisema Chenge.

Aliongeza kuwa, “Tujenge hoja maana muda ni mdogo nawaombeni tutambue kuwa tunajenga nyumba moja hivyo Mbunge Kingu endelea kuchangia. Alifafanua kuwa hakwenda bungeni kusifia tu, bali kuzungumza kuhusu upotoshaji unaofanywa kwa CCM na baadhi ya wabunge wa upinzani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3a7b015b446529c3c7b8aa60b122e7d2.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi