loader
Picha

Tanzania yaunga mkono AfDB kuongezewa mtaji

TANZANIA imeunga mkono uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kutaka kuongezewa mtaji ili itekeleze majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Saba wa Magavana ambao ni mawaziri wa fedha kutoka nchi 54 wanachama wa benki hiyo jijini hapa nchini Marekani, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alieleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndio sababu inaunga mkono kusudio hilo.

Alisema benki hiyo imeipatia Tanzania mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, kilimo, nishati na maji.

Benki inataka kuongezewa mtaji kwa asilimia 200 kutoka wastani wa UA bilioni 67.69 hadi UA 191.89 (kutoka dola za Marekani 94.76 hadi dola bilioni 268.6) ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii ya nchi wanachama hususan katika ujenzi wa reli, barabara, usafiri wa anga, tehama, bandari, uzalishaji na usambazaji wa nishati.

“Wakati umefika ili twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na benki hii yanaonekana katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika tofauti na benki nyingine,” alisisitiza Dk Mpango.

Uamuzi wa nchi za Kiafrika zenye hisa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika ya kutaka benki hiyo iongezewe mtaji, ulitolewa wakati wa mkutano wa magavana wa benki hiyo mjini Rome, Italia, baada ya mahitaji ya nchi wanachama ya kutafuta mikopo kwenye taasisi hiyo kuongezeka

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Washington D.C

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi