loader
Picha

Bakwata watoa maelekezo mapya masuala ya ndoa

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza utaratibu mpya wa ufungishaji na utoaji wa vyeti vya ndoa kwa waumini wote wa dini ya Kiislamu, huku likiwataka mashehe na maimamu waliopo katika misikiti yote nchini kuzingatia suala hilo.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma, alisema utaratibu huo mpya umelenga katika kuboresha masuala ya ufungishaji na utoaji wa vyeti hivyo kwa kuufanya kuwa mfumo mmoja rasmi wenye misingi imara na uwazi kwa manufaa ya dini hiyo, Taifa na jamii kwa ujumla.

Mruma alisema utaratibu huo unaotarajiwa kuzinduliwa rasmi leo, pia unalenga kuboresha mpango mzuri wa uwekaji wa kumbukumbu za ndoa ndani ya dini hiyo zinazofungwa na wafungishaji maalumu watakaotambuliwa kupitia mfumo huo na hivyo kuondoa mikanganyiko inayojitokeza hususani kuhusu uhalali wa wafungishaji ndoa.

“Utaratibu huu ni mwendelezo wa mipango mbalimbali inayofanywa na Bakwata kujisimamia na kujiendesha kikamilifu, hatua hii muhimu pia itahusisha utolewaji wa leseni na kitambulisho cha wafungishaji wa ndoa sambamba na kitabu cha hati za ndoa kitakachotambulika na Bakwata,” alisema Mruma.

Katibu Mkuu wa Bakwata amesema hatua hiyo imekuja miezi michache tangu kuwekwa kwa utaratibu mpya wa utambuzi wa misikiti, madrasa, walimu wa madrasa na maimamu wa misikiti kote nchini ambao pia kama ilivyo kwa wafungishaji wa ndoa, mwendeshaji hupewa leseni ya utambuzi.

“Hii ni kusema kila muoaji au muolewa kwa ndoa ya Kiislamu anapaswa kujiridhisha kama muozeshaji ana leseni na kitambulisho na ahakikishe anatoa cheti kipya ambacho kitaonesha kuidhinishwa kutolewa na muozeshaji mwenye leseni na kitambulisho husika,” alifafanua Mruma.

Vinginevyo cheti kitakachotolewa ikiwa ni cha zamani kitakuwa hakifai na ikiwa ni kipya pia kitaleta shida ikiwa hakitatolewa na mwenye leseni husika.

Alisema gharama za usajili kwa mfungishaji wa ndoa ni Sh 110,000 ikihusisha malipo kwa ajili ya fomu, leseni, kitambulisho pamoja na kitabu cha hati za ndoa.

Alisisitiza leseni hiyo kuwa inatolewa kwa shehe yeyote aliyeomba na kutimiza masharti hayo bila kujali taasisi yake huku malipo hayo yakipaswa kulipiwa benk  kwa akaunti ya Bakwata.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi